Meneja wa Masoko na Biashara wa Compact Energies Alfred Msafiri akizungumza mteja wakati alipotembelea Banda la Compact Energies kwenye Maonesho ya Utalii ya  Arusha Kili Fair yaliyofanyika jijini Arusha.

Matukio katika picha ya Compact Energies katika Maonesho ya Utalii  Kili Fair yaliyofanyika jijini Arusha.

WATANZANIA wametakiwa kuunga mkono jitihada za Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kuuhamasisha umma juu ya matumizi ya nishati mbadala ukiwemo Umeme Jua ili kutunza mazingira na kuokoa gharama za maisha.

Akiongea wakati wa maonesho ya kimataifa ya Kili Fair Arusha yenye lengo la kusaidia pia ukuaji wa sekta ya utalii, Meneja wa Masoko na Biashara wa Compact Energies Alfred Msafiri amesema Serikali kwa sasa inasimamia ajenda ya kimataifa ya matumizi ya nishati mbadala ikiwemo kuhamasisha matumizi ya majiko ya kupikia yanayotumia nishati ya gesi katika kutunza mazingira na kuzuia ukataji miti kwa ajili ya kuni.

Amesema katika kuunga mkono jitihada hizo, Compact Energies kupitia banda lake imetumia maonesho hayo kuelimisha umma juu ya matumizi ya nishati mbadala ya umeme jua ambao unapatikana kwa uhakika hapa nchini kwa sababu ya uwepo wa teknolojia ya kisasa ya uzalishaji huo na uwepo wa jua vipindi virefu vya jua kwa ajili ya kuzalisha nishati hiyo.

“Tukiwa kama kampuni ya Kitanzania, tunafurahia mazingira wezeshi ya kufanya kazi na kutoa fursa ya ajira kwa vijana na huduma bora kwa wateja wetu hapa nchini,”

“Tumewekeza katika vifaa vyenye ubora wa hali ya juu vinavyowezesha uzalishaji wa umeme wa uhakika muda wote na kutoa huduma kwa wateja wetu kwa gharama nafuu kabisa popote pale walipo,”, amesema.

“Hii ni katika kuiunga mkono Serikali ambapo kupitia huduma zetu, wateja wetu wanapata umeme jua wa uhakika na kushiriki katika ukuaji uchumi hapa nchini ,” amesema Msafiri wakati wa maonyesho hayo mkoani Arusha.

Wananchi mbalimbali walionyesha kuvutiwa na huduma za umeme jua kwa sababu ya unafuu wake ambapo mteja akifunga hakutani tena na gharama za matumizi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...