Meneja Mkaazi wa Kampuni ya EY Tanzania, Joseph Sheffu, akizungumza wakati wa kuchambua Mapendekezo ya bajeti ya Serikali ya 2024/ 2025. uchambuzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam Juni 14, 2024.
Meneja Mkaazi wa Kampuni ya EY Tanzania, Joseph Sheffu, akizungumza wakati wa kuchambua Mapendekezo ya bajeti ya Serikali ya 2024/ 2025. uchambuzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam Juni 14, 2024.
Meneja Mwandamizi wa kampuni za Mahesabu na ushauri wa kodi ya EY Tanzania Freddy Rugangila akizungumza wakati wa kuchambua Mapendekezo ya bajeti ya Serikali ya 2024/ 2025. uchambuzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam Juni 14, 2024.

Chiaru Masonobo akizungumza wakati wa kuchambua Mapendekezo ya bajeti ya Serikali ya 2024/ 2025. uchambuzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam Juni 14, 2024.

Na Avila Kakingo, Michuzi Tv
 KAMPUNI za Mahesabu na Ushauri wa kodi hapa nchini, zimesema mapendekezo ya bajeti ya serikali ya 2024/2024 imekuwa bajeti shirikishi, Serikali imejitahidi kwa kiasi kikubwa kujumuisha wadau wote katika Mchakato mzima wa ukusanyaji wa mapato.

Hayo yamesemwa na Meneja Mwandamizi wa kampuni za Mahesabu na ushauri wa kodi ya EY Tanzania, Wakili Freddy Rugangila wakati wa uchambuzi wa bajeti hiyo leo Juni 14, 2024 jijini Dar es Salaam, amesema kuwa malengo makubwa ya serikali ya kimkakati yataenda kutimia.


"Tumeona serikali imewekeza katika wigo wa kodi, pia imeweka mapendekezo mbalimbali yanayoongoza katika kuimarisha ulipaji wa kodi bila shuruti kwa walipa kodi.""Bajeti ya mwaka huu inatekelezeka hususani ukiangalia katika nyanja za Digital economy, Serikali imeleta mabadiliko haya kutoka sheria ya mwaka 2022 ambapo watu wasio wakazi wanaotoa huduma za kibiashara kupitia mitandaoni wameweza kuwa katika wigo kodi." Ameeleza Lugangila

Amesema kuwa pamoja na mafanikiohayo, serikali imewaongeza wafanyabiashara na wazalishaji wa maudhui wa ndani katika wigo wa kodi.

Pia amesema Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeweza kuwaandikisha baadhi ya makampuni makubwa yaliyopo nje ya nchi
kulipa kodi kama inavyohitajika.

Akizungumzia kuhusiana na upatikanaji wa mikopo, Wakili Lugangila amesema serikali imeweka mpendekezo ambayo yataiwezesha kupata mikopo kwaajili ya kuendesha miradi ya kimkakati hususani reli ya kisasa (SGR), uwanja wa ndege wa Dodoma, Mradi wa Magari ya Mwendo kasi kwa jiji la Dar es Salaam.

Akizungumzia kuhusiana na Waziri wa fedha akisema katika Mapendekezo ya bajeti ya 2024/2025 kuhusiana na adhabu za ajali zinazopoteza nguvu kazi kubwa ya taifa, Wakili Lugangila amesema kuwa mpango huo wa serikali utaongeza umakini kwa madereva na watumiaji wa vyombo vya usafiri barabarani.

"Ikiwezekana Serikali iweke adhabu ya kosa la jinai kwa watakaosababisha ajali kwa uzembe na kusababisha vifo vya abiria, hii tunaamini itakuwa mwarobaini wa ajali za barabarani kwani limekuwa tatizo sugu kwa kipindi kirefu." Amesema.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Ernst & Young, Joseph Sheffu amesema mapendekezo ya bajeti ni tulivu na imekuwa na uangalizi zaidi kutokana na kuelekea kwenye Uchaguzi.

Amesema mapendekezo hayo hayajaleta majonzi kwa wananchi kwani ni muda muafaka kutokana na mabadiliko ya uongozi yatakayokwenda kufanyika.

"Pia bajeti hii inania ya kuweza kukuza uchumi ukizingatia kuwa Uchumi uliporomoka kama ulivyo uchumi wa nchi nyingine, kutokana na mwaka 2019 mpaka 2020 kuwa na COVID 19 pia kuwepo kwa vita vya Urusi na Ukraini na vya mashariki ya kati.

"Tumeona uchumi umeanza kukua na umeanza kwenda juu tena kuelekea kwenye namba 7 hadi 10, kwa mwaka huu uchumi ukekuwa kwa asilimia 5.1 na bajeti hii inania ya kuongeza angalau tufikie asilimia 5.4. kwa 2025." Amesema Sheffu

Kwa Upande Chiaru Masonobo, akizungumzia uchambuzi wa mapendekezo ya bajeti serikali ya 2024/2025 amesema kuwa serikali imeweza kuwafikia watu wote katika idara ya kodi, moaka wakulima, wafugaji, wavuvi pia wameongeza kodi ya zuio ambayo hata ukinunua mahindi lazima uweze kulipa kodi ya asilimia 2 ambapo bajeti zilizopita hazikuweka mapendekezo hayo.

"Mapendekezo ya bajeti ya mwaka huu tumeyapokea vizuri tunaamini nchi yetu tunaweza kujiendesha kwa asilimia kadhaa kutokana kuongezeka kwa wigo wa ukusanyaji wa mapato kama kila mtanzania atakuwa tayari kulipa kodi." Amesema


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...