Raisa Said,Tanga

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga Husna Sekiboko leo tarehe 29 May 2024 ametekeleza agizo la Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT Mama Mary Chatanda la kuchangia Simu kwaajili ya usajili wa wanachama wa CCM na UWT.

Katika utekelezaji huo Sekiboko amekabidhi simu 10 zenye thamani ya sh. Million 4, kwa Makatibu na Wenyeviti wa Jumuiya hiyo kutoka Wilaya zote za Mkoa wa Tanga.

Hata hivyo Wenyeviti na Makatibu hao kutoka Wilaya za Tanga, Lushoto, Mkinga, Pangani, Handeni, Korogwe, Muheza, Kilindi, vijijini na Mjini walimshukuru Mbunge Sekiboko nakusema ameleta simu hizo wakati muafaka chama kikiwa na mkakati wa kusajili wanachama wengi ikiwa ni moja ya nyenzo ya ushindi wa Kishindo kwa CCM katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwakani.

Kwa upande wake Sekiboko amesema anafurahi kutekeleza agizo hilo ikiwa ni moja ya mchango wake wa kuhakikisha RAIS SAMIA SULUHU HASSAN anapata ushindi Mkubwa wa kihistoria katika uchaguzi kuu wa mwaka 2025.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...