Thobias Makoba, ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari – Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali. Bw. Makoba anachukua nafasi ya Mobhare Matinyi ambaye amepangiwa majukumu mengine. Kabla ya Uteuzi huu Bw. Makoba alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano katika Ofisi ya Majili wa Hazina.MFA

Kabla ya kujiunga na Ofisi ya Msajili wa Hazina, Bw. Makoba alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mwandamizi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Pamoja na kushiriki katika majukwaa mbalimbali ya Kimataifa ikiwemo UN, African Union, SADC, EAC, World Economic Forum na mengineyo, kwa vipindi mbalimbali aliwahi kuwa Katibu wa Mawaziri wawili wa Mambo ya Nje Bernard Membe na baadae Balozi Dokta Augustine Mahiga kabla ya Kwenda kuwa Kaimu Mkurugenzi Msaidizi katika Ofisi ya Mambo ya Nje Zanzibar.

Bw. Makoba ana Masters Degree in Security and Strategic Studies kutoka National Defence College - Tanzania, Post-Graduate Diploma in Economic Diplomacy kutoka Chuo Cha Diplomasia Kurasini na Degree ya kwanza ya Political Science and Sociology with majors in International Relations.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...