Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, na Mkurugenzi Mkazi wa TradeMark Africa (TMA), Bw. Elibariki Shammy, wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka taasisi mbalimbali zinazotekeleza miradi inayofadhiliwa na TMA baada ya kuhitimisha Mkutano wa 47 wa Kamati Tendaji ya Kitaifa (National Oversight Committee -NOC), jijini Dodoma.

Na. Saidina Msangi, WF, Dodoma.
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, ameongoza Mkutano wa 47 wa Kamati Tendaji ya Kitaifa (National Oversight Committee -NOC) inayosimamia utekelezaji wa miradi ya kuwezesha na kuboresha mazingira ya biashara nchini kwa ufadhili wa TradeMark Africa (TMA), kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Natu El- maamry Mwamba.

Mkutano huo umeidhinisha bajeti ya mwaka 2024/2025 kiasi cha dola za Marekani milion 7.1 ambayo itatekeleza miradi mbalimbali inayolenga kuongeza ufanisi wa biashara nchini na ukanda kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kujenga uwezo kwa vijana na wanawake katika kufanya biashara hususan katika Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA).

Mkutano huo pia umepokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa miradi ya TMA kwa mwaka 2023/2024 ambapo ilibainishwa kuwa kwa kipindi cha Julai 2023 - Juni 2024, miongoni mwa mafanikio ni kukamilika kwa Sera ya Biashara (National trade policy) ambayo itazinduliwa tareh 11 Julai 2024.

Mafanikio mengine ni kukamilika na kuzinduliwa kwa Mfumo wa Kieletronic wa Uwekezaji (Tanzania Investement Single Window System) ambao unawezesha wawekezaji kuomba vibali vya uwekezaji kwa njia ya mtandao.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, akiongoza Mkutano wa 47 wa Kamati Tendaji ya Kitaifa (National Oversight Committee -NOC) inayosimamia utekelezaji wa miradi ya kuwezesha na kuboresha mazingira ya biashara nchini kwa ufadhili wa TradeMark Africa (TMA), kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Natu El- maamry Mwamba, jijini Dodoma.

Afisa Biashara Mwandamizi Wizara ya Viwanda na Biashara, Bw. Mpanduji Marthias na Afisa kutoka Trade Mark Afrika Bi. Kezia Mbwamba, wakipitia nyaraka wakati wa Mkutano wa 47 wa Kamati Tendaji ya Kitaifa (National Oversight Committee -NOC) inayosimamia utekelezaji wa miradi ya kuwezesha na kuboresha mazingira ya biashara nchini kwa ufadhili wa TradeMark Africa (TMA), jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, na Mkurugenzi Mkazi wa TradeMark Africa (TMA), Bw. Elibariki Shammy, wakiwa katika picha ya pamoja na Wafadhili na watumishi wa TMA baada ya kuhitimisha Mkutano wa 47 wa Kamati Tendaji ya Kitaifa (National Oversight Committee -NOC) inayosimamia utekelezaji wa miradi ya kuwezesha na kuboresha mazingira ya biashara nchini kwa ufadhili wa TradeMark Africa (TMA), jijini Dodoma.
Baadhi ya Washiriki wakifuatilia mawasilisho wakati wa Mkutano wa 47 wa Kamati Tendaji ya Kitaifa (National Oversight Committee -NOC) inayosimamia utekelezaji wa miradi ya kuwezesha na kuboresha mazingira ya biashara nchini kwa ufadhili wa TradeMark Africa (TMA), jijini Dodoma.
Meneja wa Programu ya TradeMark Africa (TMA), Bw. Solomon Michael, akitoa ufafanuzi wa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya TMA kwa mwaka 2023/2024 katika Mkutano wa 47 wa Kamati Tendaji ya Kitaifa (National Oversight Committee -NOC) inayosimamia utekelezaji wa miradi ya kuwezesha na kuboresha mazingira ya biashara nchini kwa ufadhili wa TradeMark Africa (TMA), jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mawasilisho wakati wa Mkutano wa 47 wa Kamati Tendaji ya Kitaifa (National Oversight Committee -NOC) inayosimamia utekelezaji wa miradi ya kuwezesha na kuboresha mazingira ya biashara nchini kwa ufadhili wa TradeMark Africa (TMA), jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkazi wa TradeMark Africa (TMA), Bw. Elibariki Shammy, akitoa ufafanuzi wa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya TMA kwa mwaka 2023/2024 katika Mkutano wa 47 wa Kamati Tendaji ya Kitaifa (National Oversight Committee -NOC) inayosimamia utekelezaji wa miradi ya kuwezesha na kuboresha mazingira ya biashara nchini kwa ufadhili wa Trademark Africa (TMA), jijini Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF- Dodoma)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...