Mwenyekiti wa Chama Cha Watu wenye Ualbino Tanzania TASS ,Godson Mollel  akizungumza katika kongamano  hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson Simon  ambaye alikuwa  mgeni rasmi akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge.Na Khadija Kalili, Michuzi Tv 

WATU  wenye Ulemavu  wa Ngozi Ualbino nchini  wameiomba serikali  kuwawekea nazingira ya usalama wao  katika kuelekea  kipindi cha  Uchaguzi  wa Serikali za mitaa  utakaofanyika  baadaye mwaka huu  na Uchaguzi Mkuu ujao 2025.
 
Hayo  yamesemwa  na Mwenyekiti  wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino (TASS),
Godson Mollel  
katika  leo Juni 12  katika Kongamano  la Uelewa  kuhusu Ualbino  ambao kilele chake ni kitafanyika kesho   Juni 13.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kibaha  Mkoa wa Pwani  Nickson Simon  amewatoa hofu Chama  Cha Watu wenye Ualbino Tanzania (TAS) kwamba serikali itahakikisha inakomesha  vitendo vya  mauaji  kwa watu wenye changamoto  ya ngozi (Albino).

"Serikali  iko kazini  katika kuzuia  mauaji  ya Albino  nchini  na kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji  Abubakari Kunenge ambaye amenituma nije kumuwakilisha katika Kongamano  hili leo nasema  kuwa vitendo hivi vitakomeshwa kabisa endapo tu tutatumia  njia ya kupeana  elimu kwani tunaimani kubwa endapo jamii  wakipata ufahamu  wa kutosha kwamba vitendo vya mauaji ya Albino ni kinyume  na haki za binadamu  na kwamba  watu wote tuna haki ya  kuishi kwa misingi   ya utu,undugu na amani mauaji  haya yatakoma.

"Kitakwimu inaonesha kuwa kati ya watu 20,000 mtu mmoja anavinasaba vya Ualbino , kati ya watu1,400 mmoja kati yao ni Albino huku ndani ya Mkoa wa Pwani kuna watu 569 huku watu 368 ambao wanahudhuria Kliniki  na wanapata  misaada  mbalimbali  inayowahusu.

DC Nickson  amesema hayo  leo  wakati alipokuwa mgeni rasmi akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Pwani katika Kongamano la  Uelewa  kuhusu Ualbino  linalofanyika kwenye Ukumbi wa mikutano wa Shule ya Siasa ya Mwalimu Julius Nyerere iliyopo Kwamfipa Kibaha  Mkoani Pwani.

" Elimu zaidi  inahitajika  kwa jamii kuhusu kukwepa unyanyapaa dhidi ya  watu wenye ualbino na mauaji yatakoma pindi tu  jamii  itakapokuwa  na uelewa wa kutosha juu ya changamoto ya watu wenye Ualbino" amesema  DC Simon.

Aidha Mwenyekiti wa TASS  Godson Mollel ameiomba Mahakama kutôa adhabu kali kwa watu wanaokutwa na hatia ya kuwakata viungo au kuwaua watu wenye Ualbino.

 Mwenyekiti wa Taifa wa TAS Godson Mollel alipozungumza na waandishi wa habari wakati wa maadhimisho ya kitaifa ya siku kuongeza uelewa juu ya Ualbino (IAAD) duniani.

Mollel amesema kuwa Mahakama ikitoa hukumu kali kwa wahusika wa mauaji ya Albino itakuwa fundisho kwa watu wanaojihusisha na vitendo hivyo kuacha kuwadhuru. 

Mkurugenzi wa Kitengo Cha Huduma kwa watu Wenye Ulemavu Ofisi ya Waziri  Mkuu Kazi, Vijana Ajira na Watu Wenye  Ulemavu Rasheed  Maftah amesema kwamba serikali  inaadaa sera na miongozo mbalimbali kwa watu wenye ulemavu ili kuweka usawa.

Wakati huohuo Ofisa  Ustawi Mkuu  kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Watu wenye ulemavu Joy Maongezi amesema kuwa sheria namba 9 ya mwaka 2010 inataka kuwa na haki kwa watu wenye ulemavu ambapo watu wenye Ualbino ni sehemu yao.

Katika maadhimisho hayo  huduma mbalimbali zimetolewa ikiwa ni pamoja na upimaji saratani ya ngozi, utoaji miwani, kofia na mafuta maalumu ya kuzuia ngozi kutoathirika  na  mionzi ya jua , upimaji wa tezi dume na kansa ya mlango wa shingo ya kizazi.

Maadhimisho hayo hufikia kilele  kila ifikapo Juni 13 dunia kote  na kwa mwaka huu kitaifa yamefanyika Kibaha Mkoani Pwani.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...