Na Zainabu Hamis,
Habari njema zenye kuleta matumaini kwa wasafiri wanaotumia Bus kutoka Dar es Salaam Tanzania hadi Johannesburg ,Afrika Kusini kwa Mzee Madiba, kampuni ya kizalendo ya Usafirishaji Tanzania Mkombe Logistics yenye makao yake mjini Johannesburg,South Africa ambayo kwa sasa ndio inayo safirisha abiria kwa kutumia mabasi yake Mkombe Luxury Bus kampuni hiyo imejikuta ndio kinara wa usafiri wa barabarani kwa kupasua mipaka ya kuanzia Johannesburg, Afrika kusini kupitia Zimbabwe,Zambia hadi Dar es Salaam,Tanzania usafiri huo unawapitisha abiria katika maporomoko ya Victoria Falls umekuwa unaongoza na kuweza kuongeza idadi ya mabasi yake ambayo kila jumamosi basi moja linaondoka Dar es Salaam kwenda Afrika Kusini na basi lingine likiwa linaondoka Johannesburg hadi Dar es salaam Tanzania.

Mkombe Luxury Bus fahari ya watanzania imetajwa na vianzo vingi ndani na nje kwa kuweza kutoa uduma zake nzuri za usafirishaji wa abiria na mizigo kwani kampuni hiyo ya kizalendo pia inasafirisha mizigo kwa usafiri wa malori na Sprinter Van katika nchi za Kusini na mashariki ya Afrika.

Mamlaka za Usafiri wa nchi za Malawi,Zambia,Botswana na Zimbabwe zimeiomba kampuni hiyo hiweze pia kutoa uduma ya usafiri wa abiria kuvuka mipaka ya nchi hizo kwa maana hii Mkombe Luxury Bus imejikuta kuwa ndio kiungo cha usafirishaji wa abiria kwa njia za nchi kavu, katika wiki hizi watalii wengi wakitokea afrika kusini wamekuwa wakiingia nchi Tanzania kwa kupitia usafiri wa Mkombe Luxury Bus ambao ofisi yake kwa Dar es salaam,ipo Shekilango Road ,Ubungo business park hawa jamaa pia wanapatikana kwa What’s App at +27604749717

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...