Mradi wa USAID kizai hodari unalenga kuimarisha afya, ustawi na ulinzi wa watoto yatima, wenye mazingira hatarishi pamoja na vijana wa rika barehe wanaoishi katika jamii zilizoathirika zaidi na maambukizi ya virusi vya ukimwi.

Mradi huo unatekelezwa katika mikoa tisa ya Dodoma, Kilimanjaro, Tanga, Singida, Mwanza, Mnyara, Arusha, Mara na Geita

Issa Murshid ni Mkurugenzi mshiriki Kanda ya Kaskazini Mashariki akizungumza na waandishi wa Habari mjini Morogoro kwenye kikao kazi kilichowakutanisha waganga wakuu wa mikoa na Wilaya, Maafisa ustawi wa jamii na Mendeleo ya jamii pamoja na wadau wengine kutoka mikoa mine inayotekeleza mradi huo kanda ya Kaskazini mashariki.

Amesema kuwa mradi wa USAID kizazi hodari unatekelezwa na Kanisa la Kiinjili Kirutel Tanzania (KKKT) na kufadhiliwa na shirika la misaada la maendeleo la watu wa marekani USAID kupitia PEPFAR kwa mwaka huu unalenga kuwafikia zaidi ya kaya elfu moja

Amesema mmoja ya njia ya wanazozitumia kuwapata watoto hao ni pamoja na utambuzi kwenye vituo vya Afya, kupitia mama mjamzito wakati wa kufanyiwa uchunguzi na endapo itabainika kuwa anaambuzi ya virusi vya ukimwi, atafuatiliwa mpakam kujifungua na kujua hali ya mtoto.

Mradi unawasaidia wanufaika kujiimarisha kiuchumi kwa kuunda vikundi na kupatiwa mikopo kupitia Halmashauri na taasisi mbalimbali yenye riba nafuu pia kuhakikisha wanatumia dawa za kufubaza virusi wanazitumia kwa kufuata ushauri wa Daktari ili kuimalisha afya zao

Kwa upande wake Afisa ustawi wa jamii Mkoa wa Dodoma Josephine Mwaipopo amesema kuwa Mradi wa USAID kizazi hodari ni mradi unaowaunganisha walengwa na watoa huduma mbalimbali zikiwemo afya, elimu pamoja na taasisi za kifedha ili kuwaongezea kipato kuweza kujiinua kiuchumi, kuwawezesha watoto kufikia malengo yao.

“Kwa serikali tunasema mradi wa USAID kizazi hodari umefanya kazi kubwa sana, mpaka sasa umetimiza miaka 2 lakini umetuwezesha serikali kupata takwimu ambazo zimetusaidia kupanga mipango ya mwaka, pia zimetusaidia kupunguza changamoto za watoto ambao waliokuwa mazingira hatarishi na kupunguza ukatili wa kijinsia” Amesema Bi Mwaipopo

Happy Luteganya ni Mkuu wa idara ya Maendeleo ya jamii Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga amesema mradi wa kizazi hodari kwa Korogwe unatekelezwa katika kata 11 umesaidia kuibua watoto wanaofanyiwa ukatili wa kijinsia pia mradi umeweza kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira hatalishi kuinuka kiuchumi kupitia familia zao kwa kuwaunganisha na taasisi za mikopo kwa kuunda vikundi na kuweza kujiunua kiuchumi. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...