SEKTA ya huduma za fedha ni miongoni mwa sekta zinazokua kwakasi hapa nchini, huku ujumishaji wa watu katika huduma hizo muhimu za kiuchumi ukiongezeka.

Katika kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali za kuhakikisha Tanzania inaendana na Mapinduzi ya Kiuchumi kwa kuhakikisha wananchi wanajiunga na kutumia mifumo rasmi ya kibenki, Benki ya Equaity imezindua rasmi mfumo mpya wa kiteknlojia wa kufungua na kupata akaunti rasmi za benki hiyo kwa njia ya simu.

Mfumo huo unatajwa kuwa rahisi na haraka na wenye kuendana na mapinduzi ya Sayansi na Teknolojia katika mageuzi ya mifumo ya kidigitali katika uchumi wa nchi, huku ikilenga kuleta mabadiliko ya njai ya ufunguzi wa akaunti wa hapo awali.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma ya ‘ Hapo Hapo’ Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Malipo Benki ya Equity Aidan Chamshama, amesema huduma hii inamuwezesha mtanzania kufungua akaunti ya Equity popote alipo bila kufika katika tawi, na kujaza fomu, kwa kigezo cha kuwa na namba ya Nida kwa kutumia simu ya mkononi.

Kwa upande wake Meneja benki ya Equity tawi la Mbagala, Salum Halfani amesema akunti hiyo inayofunguliwa kwa njia ya simu ndani ya masaa 24 inatoa huduma zote za kibenki ndani na nje ya nchi.

Mteja wa benki hiyo Teresia Luzige, amesema ufunguzi wa huduma hiyo utarahisiha upotevu wa muda wa kwenda kwenye tawi kufungua akaunti .








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...