Waziri Mkuu Kassim Majakiwa amesema Serikali inaendelea kujikita katika kuhakikisha inaimarisha na kuwashirikisha wavuvi na wafugaji katika mipango ya maendeleo.

Amesema hayo leo Juni 03, 2024 alipoweka jiwe la msingi la ujenzi wa soko la samaki la kisasa la Chato Beach, Chato mkoani Geita.

Amesema kuwa Mradi huo unaotoa fursa kwa yeyote aliyeanza na anayetaka kujikita kwenye sekta ya uvuvi kunufaika na kujiingizia kipato. “Kitendo cha Serikali kuleta soko hili hapa ni kuhakikisha wanasogeza fursa kwa wavuvi wa eneo hili, soko hilo ni lenu, imarisheni uchumi wenu kupitia soko hili”.

Ameongeza soko hilo litakuwa na uwezo wa kukausha hadi tani 10 za dagaa kwa siku kwa kuwa kutawekwa mtambo wa kukausha samaki. “Tutaweka mafriji makubwa mawili ya kutunzia samaki, pamoja na chumba maalum cha kuzalisha barafu”

Ujenzi wa soko hilo ambalo umefikia asilimia 90 utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.75 na utasaidia kupunguza upotevu wa samaki hasa dagaa baada ya kuvunwa, kuongeza thamani ya mazao ya uvuvi, kutoa ajira zipatazo 1473 kwa wavuvi, wafanyabiashara na wachuuzi na kuimarisha ukusanyaji wa takwimu za uvuvi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...