Na: Josephine Majura na Asia Singano WF, Dodoma.
Umoja
wa Wanawake wa Wizara ya Fedha, (Golden Women), wameshauriwa kuendeleza
utamaduni wa kutoa misaada mbalimbali kwa watu wenye mahitaji maalumu
ili kuwasaidia kufikia malengo yao.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi Jenifa Christian Omolo, ametoa ushauri
huo alipotembelea Kituo cha Huduma cha SAFAAD, kilichopo Kijiji cha
Membe, Wilayani Chamwino mkoani Dodoma.
Aliongeza
kuwa kuwakumbuka watu wenye mahitaji mbalimbali ni jambo zuri hivyo ni
vema utaratibu huo ukaendelea ili kuhakikisha wanawafikia makundi
mbalimbali ya watu wenye uhitaji.
"Niwapongeze
Uongozi wa Golden Women kwa umoja wenu wa kujitoa kwa hali na mali na
kuhakikisha zoezi hili linafanikiwa”alisema Bi. Omolo
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Wizara ya Fedha Bi.
Consolatha Maimu, aliahidi kuendelea kuwahamasisha Wanakikundi hao kuwa
na utaratibu wa kuwasaidia watu wenye mahitaji mbalimbali.
Naye
Mkuu wa Kituo cha Huduma cha SAFAAD, Bw. Adolph Alfred, aliwashukuru
Wanawake wa Kikundi cha Golden Women kwa kufika Kituoni hapo na kupeleka
mahitaji .
Naye
mmoja wa wanufaika wa mahitaji hayo Bi. Florentina Aloyce, aliuomba
uongozi wa Kikundi cha Golden Women, kuendelea kuwa mabalozi kwa vikundi
vingine ili viweze kufika kituoni hapo ili waweze kupata mahitaji kwa
kuwa bado wana mahitaji mengi.
Katika
kuelekea maadhimisho ya sherehe ya Umoja wa Wanawake, Wizara ya Fedha,
imetembelea Kituo cha Huduma cha SAFAAD kwa ajili ya kupeleka mahitaji
ikiwemo mahitaji ya shule, vyakula, vinywaji na mahitaji mengine
mbalimbali.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara
ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, akikabidhi zawadi kwa Mkuu wa
Kituo cha Huduma cha SAFAAD, Bw. Adolph Alfred, kwa niaba ya Kikundi cha
Umoja wa Wanawake wa Wizara ya Fedha (Golden Women) walipotembelea
kituo hicho na kutoa mahitaji mbalimbali, kuelekea kilele cha Siku ya
Wanawake tarehe 14 Julai, 2024.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara
ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo (wakwanza kushoto), akiteta jambo
na viongozi wa Kikundi cha Umoja wa Wanawake wa Wizara ya Fedha (Golden
Women), walipotembelea Kituo cha Huduma cha SAFAAD, kilichopo Chamwino
mkoani Dodoma, katikati ni Mwenyekiti wa Golden Women Bi. Consolatha
Maimu na Katibu wa kikundi hicho Bi. Nyanzala Nkinga.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara
ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, akizungumza na baadhi ya watumishi
wanawake wa Wizara ya Fedha, Wamiliki wa Kituo cha Huduma cha SAFAAD,
walezi na watoto wanaolelewa katika kituo hicho, kilichopo Chamwino
Mkoani Dodoma baada ya kutembelea na kutoa mahitaji mbalimbali ikiwemo
vyakula, vinywaji, nguo, fedha taslim na mahitaji mengine.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara
ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo (wakwanza kulia), akizungumza na
Viongozi wa Kituo cha Huduma cha SAFAAD, kilichopo Chamwino mkoani
Dodoma, baada ya kutembelea kituo hicho, wakwanza kushoto ni Mkuu wa
Kituo cha Huduma cha SAFAAD, Bw. Adolph Alfred pamoja na Bi. Joan
Abdallah.
Naibu
Katibu Mkuu,Wizara ya Fedha , Bi. Jenifa Christian Omolo (wapili kulia),
akizungumza na baadhi ya Watoto, Frolentina Aloyse (watatu kulia) na
Sharifa Sungura (wanne kulia), wanaolelewa katika Kituo cha Huduma cha
SAFAAD, kilichopo Chamwino mkoani Dodoma baada ya kutembelea kituo
hicho.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha - Dodoma)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...