Mwalimu wa Urembo Chuo VETA Shinyanga  Judi Mwita akionesha umahiri wa kunyoa kwenye Banda la VETA.

*Kusema kazi za wanaume ni ndio kufanya kuwepo kwa mfumo dume.

Na Mwandishi Wetu  

MWALIMU wa Urembo wa Chuo cha VETA Shinyanga Judi Mwita  amesema kuwa wasichana wajifunze masuala ya Urembo ikiwemo unyoaji nywele za kiume kutokana na kuwepo kwa soko kubwa ya wahitaji wa huduma hiyo.

Mwita ameyasema hayo katika Banda la VETA katika Maonesho ya 48 Biashara Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.amesema hata yeye hakuamini kama anaweza kunyoa aina tofauti ya nywele za kiume lakini ameweza na kuwa Mwalimu baaada kusoma taaluma mafunzo ya Ufundi Stadi.

Judi amesema kuwa kitendo cha wanawake kubagua kazi kwa kusema wanaweza wanaume kunawapotezea fursa nyingi za kujiendeleza kiuchumi.

"Hatuwezi kuacha kufanya kazi katika vizingizio vya kuwa kazi zingine wanaweza wanaume hapana tunatakiwa wanawake tujitume na hiyo ndio inaondoa mfumo dume" amesema Judi

Hata hivyo amesema kuwa katika kipindi cha sasa Teknolojia imekuwa kubwa vitu vingi vimerahisishwa na kufanya kutokuwa changamoto ya wanawake kutofanya.

Judi amesema kuwa kazi ya Urembo inalipa kwani watu wanataka kupendeza wakati wote hivyo mtu akipata mafunzo ajira yake iko mikononi mwake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...