Na Pamela Mollel,Arusha
Tanzania imeweza kutengeneza na kuuza nchi za nje Zaidi ya mashine 1100 za teknolojia ya kilimo kutoka Kampuni ya Imara Technology ya jijini Arusha inayoendeshwa na kijana mzalendo Alfred Chengula.
“Baada ya kuwezeshwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia nchini (COSTECH), Imara Tech tumefanikiwa kuunda mashine na zana mpya za teknolojia ya kilimo zinazowezesha ufanisi wa kazi shambani hadi baada ya mavuno,” alisema Chengula katika maonesho maalum ya uzinduzi wa baadhi ya mashine mpya kutoka taasisi hiyo.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo wa Imara Technology, kampuni hiyo mpya ya jijini Arusha imeweza kuuza mashine zake bunifu zilizoundwa mkoani Arusha kwenye nchi sita za Afrika, ikiwemo Kenya, Uganda, Burundi, Malawi, Zambia na Zimbabwe.
Hata hivyo, Chengula amebainisha kuwa wazalishaji wa bidhaa za teknolojia wanakumbwa na changamoto ya gharama kubwa za kuagiza malighafi kutokana na kodi, huku akiiomba serikali iliangalie suala hilo.
Akizungumza katika maonesho hayo Mkurugenzi mkuu wa Tume ya Saynsi na Teknolojia, Dk Amos Mhunda Nungu amesema kuwa Tume hiyo imewekeza kwenye miradi Mia tatu na hamsini na nne (354) inayotekelezwa nchi nzima.
“Miradi hii inahusisha utafiti, kuendeleza miundombinu ya utafiti, uendelezaji wa teknolojia za wabunifu, kongano za ubunifu, pamoja na kumbi za ubunifu,” alifafanua Dk Nungu na kuongeza kuwa miradi hiyo imechangia kuibuka kwa teknolojia mpya pamoja na uwekezaji wa ndani, hususan miongoni mwa vijana nchini.
“UWEKEZAJI huu umechangia kuboresha mazingira ya utafiti na ubunifu, kukuza na kuhamasisha ushiriki wa wadau wengi katika utafiti na ubunifu pamoja na matumizi ya matokeo yatokanayo na utafiti na ubunifu katika sekta mbalimbali,” aliongeza mkurugenzi wa COSTECH.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omar Kipanga ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika maonesho hayo ameahidi kufanya vikao na waziri husika, mamlaka ya mapato pamoja na waziri wa fedha ili kujadili jinsi watakavyoweza kupunguza kodi kutoka malighafi zinazoagizwa kwa ajili ya viwanda chipukizi nchini.
“Na hasa wabunifu wa teknolojia zinazochangia uzalishaji, hususan kilimo cha biashara,” aliongeza Naibu waziri.
Wakati huo huo kampuni ya Honda ya Japani imesaini makubaliano maalum na Imara Technology kwa ajili ya ushirikiano katika masuala ya kuendeleza teknolojia ya kilimo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...