MAKAMU Mwenyekiti - Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, mgeni rasmi Katika uhusiano kati ya Tanzania na India
"Lengo letu katika kufanikisha tamasha hili ambalo linafanyika kwa mara ya pili. Malengo yetu ni Kwanza, kuhamasisha marafiki zetu, familia,na majirani kuzingatia mafundisho ya Krishna na kuelewa kanuni za ulimwengu na Kihindu.
Shree Goverdhannathji Haveli yafanya tamasha la siku tatu kwa ajili ya kuonyesha maisha ya Kiimani na, mafundisho ya Shree Goverdhannathji Haveli na yafanya tamasha la siku tatu kwa ajili ya kuonyesha maisha ya Kiimani, mafundisho ya Bw. Krishna ambayo yamewaleta pamoja jamii ya Kihindu kutoka kote Tanzania kwa kupitia tukio la kipekee la kitamaduni.
Shree Krishna Vaibhavam II, Hadithi Isiyosimuliwa ya Bwana Krishna, hatimaye ipo tayari kwa tamasha la siku tatu kuanzia Julai 5 hadi 7 katika Ukumbi wa Super Dome, Masaki jijini Dar es Salaam.
Katika uzalishaji na utengenaji wa hadithi hii ulianza kama ndoto miaka miwili iliyopita, baada ya tamasha la jukwaa lililofanya vizuri la Shree Krishna Vaibhavam lililofanyika kuanzia Julai 8 hadi 10, 2022 katika Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Kwa kipindi cha miezi 20 iliyopita, timu ya washiriki 150, ikiongozwa na Bi. Priti Punatar na Bi. Sonal Ganatra, wamefanya kazi kwa bidii ili kufanya tamasha hili la leo kutokea
na kufanyika katika ukumbi wa Super Dome Masaki, ukumbi ambao zinafanyika burudani zenye hadhi kubwa zaidi nchini Tanzania.
Kama alivyosema Bw. Yogesh Manek, Mwenyekiti wa Shree Goverdhannathji Haveli,
"tunajivunia kufanikisha tamasha linalosimulia hadithi takatifu kupitia aina za ngoma za kitamaduni kutoka India kwa hadhira ya Tanzania, kukuza uelewa wa kitamaduni na kuthamini umoja kati ya nchi hizi mbili."
Pili, kuhamasisha vijana wetu kushiriki katika utamaduni wetu na kuwapa uelewa wa kina wa maadili na mafundisho ya Kihindu kupitia maisha ya Bwana Krishna duniani.
Tatu, kushiriki hadithi nzuri na Watanzania, na marafiki wa Tanzania.
Na hadithi hii itapatikana duniani kote kupitia Kituo cha YouTube cha Shree Goverdhannathji Haveli mnamo Julai 7, 2024.
Kile kinachofanya tamasha hili kuwa maalum ni kwamba ni kazi ya upendo ushirikiano wa vipaji vya kucheza ngoma na muundo wake wa utengenezaji kwa kushirikiana na timu za mbalimbali zilizofanikisha hadithi hii kutoka India – chini ya uongozi na msaada wa Shree Goverdhannathji Haveli na wadhamini, wafadhili ambao kiukweli bila uwepo wao uzalishaji huu usingewezekana.
Tamasha hili linawaleta pamoja watu kutoka kila sehemu wenye maisha, umri, na jamii ya India, kwa upendo wetu wa pamoja kujifunza kuhusu maisha ya Kiimani ya Bwana Krishna. Kuhusu Shree Goverdhannathji Haveli, Tanzania.
Ilijengwa mnamo mwaka 2017, Shree Goverdhannathji Haveli, Dar es Salaam, imekuwa kituo kikuu cha utamaduni na shughuli za kidini kwa wafuasi wa Pushtimarg kwa waumini wote wa
Afrika Mashariki. Shrinathji ni umbo la Mungu wa Kihindu, Bwana Krishna aliyetokea kama mtoto wa miaka saba. Shrinathji ni mungu wa Dhehebu la Vaishnav linalojulikana kama Pushtimarg maana yake (Njia ya Neema) iliyoanzishwa na Shri Vallabhacharya Shri
Mahaprabhuji mwaka 1492 BK.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...