Na Mwandishi Wetu

Spika Mstaafu na Kamisaa wa Sensa Anne Makinda Amesema kuwa matokeo ya Sensa ndio yanatumika katika kupanga mbalimbali ya mahitaji katika jamii.

Makinda ameyasema hayo katika Banda la NBS katika Maonesho ya 48 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa wananchi waendelee kufatilia matokeo ya Sensa na kuangalia vipaumbele vinavyohitajika kutokana na matokeo hayo.

Aidha amesema kazi ya Sensa umefanyika katika maeneo matatu ambapo kwa matokeo ya Sensa ndio picha yake kwendana na mipango Serikali katika kupanga mipango yake.

Amesema kuwa kuna wakati kuna watu walipelekewa huduma wakiwa na idadi ndogo ambapo waliokuwa idadi kubwa wakaachwa ambao waliifuata huduma kwa watu wenye idadi ndogo.

Hata hivyo kwa Sensa iliyofanyika na matokeo yake Serikali itapanga mipango Kutokana na matokeo ya Sensa bila kutoa upendeleo wowote.

Makinda Kutokana na hali hiyo, amesema kuwa ipo haja ya matokeo hayo kuanza kutumika kama dira ya kupanga mipango ya maendeleo kwa Taifa kuanzia katika ngazi ya chini kutokana na idadi ya watu walipo katika maneo yao.

Makinda amesema kuwa wananchi watembelee Banda la NBS kupata taarifa mbalimbali na machapisho ya Sensa.
 

Spika Mstaafu na Kamisaa wa Sensa Anna Makinda akipata maelezo katika Banda la NBS katika Maonesho ya 48 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...