Wadau wa michezo wametakiwa kuwekeza kwa wingi katika sekta ya hiyo ambayo kwa sasa imekuwa chanzo cha ajira, furaha na kwa vijana wengi wa kitanzania .

Agizo hilo amelitoa leo Julai 6, 2024 Dar es salaam na Msajili wa vyama vya michezo kutoka katika baraza la michezo Tanzania Evord Kyando katika uzinduzi wa klabu ya mchezo wa kuogelea @Oasisi _Swimming clabu Village iliyopo Mbezi Beach amesema michezo yote ina umuhimu kwa kila mtu na hakuna wa kudharau mchezo wa mtu mwingine.

"Nisisitize kuwa mchezo wowote kwanza huimarisha viungo na kusaidia afya ya mwili laki soka, siyo bao hivyo michezo ya kuogelea aina yote ya imekuwa f Muhimu kuunganisha watanzania hali kudumisha mshikamano na amani upendo" amesema Kyando

Hata hivyo Kyando amewasihi watanzania kupenda na kuibua vipaji mbalimbali na kuendeleza michezo kwani serikali imetengeneza mazingira wezeshi

Naye Mkuu wa michezo wa Oasis Swimming Club kharid Lusheki amesema lengo la kuanzisha klabu hiyo ni kuwasaidia watanzania kuupenda na kuibua vipaji katima mchezo wa kuogelea ili kuongeza ushindani mchezo kitaifa na kimataifa

Aidha wito umetolewa na Bwa Lesheki kwa serikali kuangalia kwa jicho la umakini kuondoa kodi katika vifaa vya michezo ili hata wale wanaopenda michezo waweze kumudu ghramama kununua.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...