KUIGUSA jamii ni suala ambalo Meridianbet wamelipa nafasi kubwa ambapo leo wamehakikisha wanaendelea kuishi kwenye misingi yao, Kwani wamefanikiwa kufika maeneo mawili ndani ya jiji la Dar-es-salaam na kutoa msaada.
Meridianbet wamefanikiwa kufika eneo la Kawe Sokoni pamoja na Mbezio Afrikana ambapo wametoa msaada, Jambo ambalo limeendelea kuonesha namna mabingwa hao wa michezo ya kubashiri wamekua wakiigusa jamii kwa mrengo chanya.
Meridianbet wamefika soko la Kawe leo na kutoa vifaa vya usafi kama Mafagio, Mabuti ya kufanyia usafi, Barakoa, na Gloves, Lakini pia walifanikiwa kutoa Reflectors kwa Bodaboda wa eneo la Mbezi Afrikana na kwajili ya kuwasaidia kiusalama zaidi.
Bashiri michezo mbalimbali ambayo imepewa ODDS BOMBA pale Meridianbet wikiendi hii Bashiri sasa uweze kushinda mkwanja mnene.
Kaimu wa kitengo cha Mawasiliano na masoko kutoka kampuni ya Meridianbet bwana Abubakar Kulindwa alikua sehemu ya uwakilishi wa Taasisi hiyo kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa na alifanikiwa kuzungumza machache”Ni furaha yangu kuwepo mahali hapa kuhakikisha zoezi hili la kutoa vifaa hivi vya usafi linaenda vizuri ambapo natambua vitasaidia kuimarisha usafi katika soko hili”.
Wenyekiti wa mtaa wa Mbezi Afrikana na Kawe pia walipata fursa ya kuzungumza machache hawakua na mengi ya kusema zaidi ya kutoa shukrani kwa Meridianbet kwa kuhakikisha wanaendelea kurudisha kwenye jamii yao, Lakini zaidi wakiwasihi Meridianbet wasiache kugusa jamii zenye uhitaji kila mara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...