Rais na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ashiriki Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa katika Mji wa Serikali Mtumba Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiweka silaha za Asili (Mkuki Ngao) na shada la maua kwenye mnara wa Mashujaa wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa. Maadhimisho hayo yamefanyika katika Uwanja wa Mashujaa uliopo kwenye Mji wa Serikali Mtumba Mkoani Dodoma tarehe 25 Julai, 2024.
. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Uwanja wa Mashujaa uliopo Mji wa Serikali Mtumba Mkoani Dodoma kwa ajili ya kushiriki Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa tarehe 25 Julai, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama kwa ajili ya heshima ya Wimbo wa Taifa na ule wa Afrika Mashariki wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye Mji wa Serikali Mtumba Mkoani Dodoma tarehe 25 Julai, 2024.



Matukio mbalimbali pichani wakati wa maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma tarehe 25 Julai, 2024.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...