SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limeshukuru wadau kwa kutambua mchanguo wao katika utoaji huduma bora kwa wananchi na kupelekea kupata tuzo ya mtoa huduma bora iliyotolewa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya 48.ya biashara ya kimataifa.

Akizungumza mara baada ya kupata tuzo hili Afisa masoko TANESCO makao makuu Innocent Lupenza amesema tuzo hiyo kwao imekuwa na maana kubwa kwani imetambua mchango mkubwa unaotolewa na shirika hilo katika kuhudumia umma.

"Pamoja na changamoto ndogo ndogo ambazo tunaenda kuzimaliza tunafurahi kuona mchango wetu umeweza kutambuliwa",Amesema Lupenza.

Amesema Tuzo hiyo imeongeza morali kwa wafanyakazi kwa kuendelea kufanya kazi bora na nzuri katika kutoa huduma kwa umma.

"Tunashukuru uongozi kwani unatuwezesha kwa yale yote tunayoyataka ili kurahisisha huduma bora kwa wateja wetu",Amesema.

Sambamba na hayo Lupenza amesema kupitia huduma ya Jisoti ambayo inatolewa na shirika hilo inamsaidia mwananchi kuweza kupata huduma zote na kuripoti changamoto yeyote ya umeme pindi inapojitokeza.

"Sasa hivi tunekuja na huduma ya Jisoti ili kumsaidia mteja kupata huduma zetu na kuripoti changamoto ya umeme kwa kutumia simu yake ya mkononi kwa kutumia namba 0748550000",Amesema.

Aidha ametoa rai kwa wananchi kutembelea banda lao lililopo ndani ya viwanja vya maonesho saba saba ili waweze kupata elimu kuhusu miradi mbalimbali inayotekelezwa na shirika ukiwemo mradi mkubwa wa bwawa la Mwalimu Nyerere.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...