MONICA amefariki siku ya Jumanne tarehe 16/7/ 2024 jijini Dar es salaam baada ya kuugua Saratani kwa mida Mrefu, na kuzikwa Jumamosi July 20, 2024 huko Marangu Moshi amefariki akiwa na umri wa miaka 63
Wengi walioishi Dar es Salam mwishoni mwa miaka 1980 Hadi 1990 walimfahamu au kumsikia Mamii Kwa umaarufu wa kupika keki za harusi na kupamba kumbi za harusi Kwa ustadi mkubwa Kwa kutumia maua ya Roses, vitambaa na mapambo mengine ya kuvutia, amedumu Kwa kazi hiyo Kwa zaidi ya miaka 30
Ikumbukwe kabla ya Mamii kutambulisha utaratibu wa keki na kupamba ukumbi sherehe nyingi zilikua zikifanyika bila kipengele cha keki, mfano utaratibu wa kusherekea Birthday siku ya kuzaliwa wengi walisherekea Kwa kula chakula kizuri, au kutoka kwenda kutembea mahala wapendapo, na wengi wao hawakua wakisherekea kabisa siku ya kuzaliwa ilipita kama siku nyingine yoyote na wengine wasikumbuke hata siku yao ya kuzaliwa Kwa kusikia ahh kumbe ilikua wiki iliyopita, Jambo ambalo limekua tofauti kabisa Kwa miaka ya sasa , kuhusu mapambo ya ukumbi, sherehe nyingi zilikua zikifanyika majumbani kwenye eneo la kutosha waalikwa, utaratibu wa kufanyia ukumbini ulikua Kwa wingi na haraka baada ya wengi kuvutiwa na upambaji.
Mamii alibadilisha mtazamo mzima wa watu kusherekea sherehe zao huku wakiwiwa na kuhusisha keki ikiwa kama tukio muhimu la tukio, atakumbukwa daima Kwa kusababisha mabadiliko ya tabia ya watu kwenye kusherekea matukio
Mitindo ya keki mingi aliyoitambulisha Mamii kwa kuonyesha kipaji chake adimu ni keki zenye maumbo tofauti ikiwemo keki za muonekano wa Kanisa.
Toleo la keki za ngazi Tatu,Tano na Sita zenye Nakshi na maua.maridadi na vifungashio madhubuti, zilivuma sana miaka hiyo wanandoa wengi waliofunga ndoa miaka ya mwishoni mwa themanini na mwanzoni mwa miaka ya tisini watathibitisha hilo
Kumbukumbu za picha za Maharusi wa miaka hiyo mpaka sasa zinathibitisha umahiri wa monica kwenye taaluma ya kupika keki na kuzipamba,
Miaka ya nyuma hadi 1980 Jiji la Dar, keki kwa ajili ya sherehe kama harusi, mahafali, Ubatizo, Maulidi, na kadhalika ilionekana ni taaluma ya watu wenye asili kihindi, au waarabu. Aidha Keki zilipatikana kwa kutoa Oda Katika Hoteli kubwa za Nyota Tano kama Kilimanjaro Hotel, New Africa Hotel au Hoteli za ufukweni zikiwemo Kunduchi Beach Hotel, Bahari Beach Hotel nk, kwa unadra keki zikipikwa na masista Katika baadhi ya Parokia
Ndafu Ilikuwa ndiyo ilikua ikitumika Kwa baadhi ya sherehe kama keki Maalumu kulishana kwenye sherehe kubwa, haikuwa kawaida kuona keki za ngazi tatu au zaidi kipindi hicho na pale ilipolazimu kutumia keki, Maarufu zaidi zilikuwa za ngazi moja ifikapo kipengele cha keki
Monica Mamii!, Alileta Mapinduzi makubwa kwenye tasnia hii kwa kuanza kupika keki Kwa ustadi mkubwa zenye mapambo yanayo endana na tukio husika,
Jina lake lilivuma na kupata umaarufu katika Jiji la Dar es salaam na kusambaa viunga vya jiji hadi mikoa ya Moshi na Arusha na nchi ya jirani kama Kenya.
Kwa miaka ile kama keki ya harusi yako haikupikwa Kwa Monica Mamii Basi harusi yako sio ya kishua, kwa sasa ungesema harusi Haina kiki, uwepo wa keki ya Monica kwenye harusi au sherehe yoyote ilichukuliwa ni Jambo special na ilipaisha tukio Lako Kwa kiwango cha juu
Umaarufu wake ulikuwa kwa kasi alipoanza kupika keki zenye mfano wa Kanisa lenye paa ndefu, misalaba na kengele zenye mpangilio makini wenye muonekano maridadi hapo ndipo alijizolea Sifa kem kem, hasa kwenye sherehe za kidini mfano Ubatizo, Kipaimara, Upadrisho, Harusi, nk
Keki za Monica Mamii zilipamba matukio mengi ya kiserekali, kichama, kibalizi na hata sherehe binafsi za viongozi wa Chama na Serikali nchini Tanzania, viongozi wa kigeni, ziligusa matukio mengi ya kijamii, mfano kutiana moyo, uchumba, kupokea mgeni, Birthday party, kumtoa Mwali ndani, pongezi za kazi, mtoto, promotion, biashara, Sunna nk
Monica mbali na upishi wa keki alikua pia mpambaji mzuri wa kumbi za sherehe, mambo haya mawili alikua akiyafanya sambamba na Kwa ustadi mkubwa sana,
Ikumbukwe kabla ya Mamii kuibuka na upambaji, Ilikuwa ni sharti kuchagua ukuta mmoja ambao wahusika watakaa na ulipambwa Kwa kutumia kanga au Mkeka
Pengine mapulizo au karatasi nyembamba zenye rangi rangi, hata makuti ya minazi au maua ya makopo, hupangwa Kwa ustadi kiweko na muonekano wa kupendeza, Kwa wengine ilikua ukuta unapakwa chokaa au rangi Basi meza kuu inaandaliwa hapo
Mamii alikua ndiye muanzilishi wa Kwanza hapa jijini kuanza kupamba eneo la meza kuu Kwa kutumia maua ya Roses akichanganya na mengine akiongezea vitambaa vyenye rangi maalum na kusababisha muonekano tofauti kwenye meza kuu
Akajiongeza mbele zaidi Kwa kupamba ukumbi mzima, hapo ndiyo ilikua mwanzo wa watu wengi kuanza kufanyia sherehe za harusi na nyinginezo kwenye kumbi za sherehe.
Hii ni kutokana na kuvutiwa na mapambo aliyokua akifanya Mamii.
Uanzilishi wake wa biashara ya keki na kupamba kumbi za sherehe, ulisaidia wengi kwa kuiga mfano wake na kuanza kujiajiri Kwa kazi ya kupika keki na kupamba ukumbi.
Leo hii wengi wamefaidika na kujiajiri kama wapika keki au wapamba ukumbi.
Karakana na shughuli zake za mapishi na mapambo ya keki ilikua Maeneo ya Temeke mwisho mkabala na Bar maarufu ya Bulyaga
Monica atakumbukwa daima kama muanzilishi wa biashara ya keki za sherehe ndani ya Jiji la Dar, na kubadilisha utamaduni mzima wa jinsi ya kusherekea matukio tofauti, Leo hii imekua Jambo la kawaida kukata keki siku ya birthday zao, Leo hii kumbi za maharusi zinapambwa Kwa mitindo mizuri kabisa ya kupendeza, yote hiyo ikiwa uanzilishi wake Monica Mamii!
Nguli huyu wa kupamba kumbi za sherehe ameacha alama kubwa kwenye Tasnia ya upambaji na Taifa letu la Tanzania, kama muanzilishi mpika keki Mahiri na kupamba kumbi za sherehe katika Jiji hili kubwa la Dar es salaam na mikoa ya Tanzania na nje ya Tanzania.
Mungu ailaze peponi roho yake
Amen!
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...