-Katika Mwaka wa Fedha 2023/24 imekusanya bilioni 753

Tume ya Madini imevunja rekodi ya makusanyo ya Maduhuli ya Serikali tokea kuanzishwa kwake baada ya kukusanya kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 753 kwa Mwaka wa Fedha 2023/24 ukilinganisha na kiasi cha shilingi bilioni 678 kilichokusanywa Mwaka 2022/23.

Hayo ameyasema Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, wakati akifungua Bonanza la Michezo lililoandaliwa na Tume ya Madini katika Viwanja vya Kilimani jijini Dodoma.

Aidha, Waziri Mavunde amewataka watumishi wote wa Tume ya Madini kuendelea kuchapa kazi kwa bidii, ufanisi na kuongeza ubunifu ili kuongeza makusanyo ya maduhuli na kuisaidi nchi katika kuleta maendeleo endelevu.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameanza kwa kumpongeza Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Madini Mha. Yahya Samamba kwa kuteuliwa na kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na kuwapongeza watumishi wa Tume hiyo kwa kujitokeza kwa wingi katika bonanza hilo lenye lengo la kuimarisha afya na umoja kwa watumishi.

Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Mha Samamba amewapongeza watumishi wote wa Tume ya Madini kwa kumpatia ushirikiano wa kutosha katika kipindi chote alipokuwa akihudumu katika Tume hiyo na kuwataka watumishi wote kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza tija na kuleta manufaa kwa Taifa.

Bonanza hilo lenye lengo la kuimarisha umoja kwa watumishi wa Tume ya Madini limeshirikisha mazoezi ya viungo, mpira wa miguu, kuvuta kamba na kukimbia na magunia ambapo washindi wamekabidhiwa tuzo na zawadi mbalimbali.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...