Tume ya Umwagiliaji pia inajenga maghala mawili; moja kwa akili ya kuhifadhi mpunga na mchele; na kingine kwa ajili ya kuwekwa mashine ya kukobolea mpunga. Aidha, Waziri Bashe ameilekeza Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kuhakikisha kuwa inajenga nyumba kwa Maafisa Ugani wa Kata husika; na kujenga mifereji ya maji na barabara.
Imeelezwa kuwa, katika Mkoa wa Katavi eneo linalofaa kwa kilimo ni hekta 124,761; ambapo kuna skimu za umwagiliaji 15 zimeshasajiliwa; miradi 12 inafanyiwa upembuzi yakinifu. Aidha, miradi 2 ipo katika eneo la Kamage na Mwamkulu kwa gharama za zaidi ya Shilingi Bilioni 50; ambapo hadi sasa asilimia 22 za ukarabati umefanyika.
Miradi hiyo ni hekta 2,500 eneo la Kabage; na hekta 3,000 eneo la Mwamkulu. “Litakuwa jambo la kusikitisha endapo miundombinu itakuwa inaharibiwa. Tulinde miundombinu kwa kuchangia mfuko wa maendeleo ya umwagiliaji ili ule mfuko usaidie kukarabati marekebisho yatayojitokeza katika skimu za umwagiliaji na miundombinu yake,” amesisitiza Waziri Bashe
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...