Na Khadija Kalili, Michuzi TV
WAZIRI wa Ardhi  Nyumba na Maendeleleo ya makazi   Jerry Silaaa  amesema kuwa siku tatu za Kliniki ya Ardhi iliyoendeshwa ndani ya Halmashauri  ya Chalinze  Mlandizi na Bagamoyo  na Kibaha Vijijini amebaini kuna migogoro  sugu  ndani ya Halmashauri hizo.
Waziri Silaa amesema  hayo leo Julai 4 alipokua  katika Kliniki ya Ardhi inayoendelea Halmashauri  ya Bagamoyo  ambapo amesema kuwa Kibaha Mjini na Vijijini  huku akiyataja mashamba ya Mohammed  Enterprises  yaliyopo katika vijiji vya Soga , Kipangege yaliyopo Kihaha Vijijini kuwa yanahitaji kuchunguzwa kwa utaalamu zaidi hivyo ameacha maagizo kwa  wataalamu wake ambao watayafanyia uchunguzi  kwani vijiji hivyo vinahistoria yake wakati vilipoanzishwa  katika oparesheni anzisha vijiji kati ya 1950 na  1972
Maeneo mengine yenye migogoro  ya muda  mrefu ni pamoja na Chamakweza iliyopo ndani ya Halmashauri  ya Chalinze Wilayani Bagamoyo ambapo wakulima na wafugaji kila mmoja akidai kuwa ndiye mmiliki  halali wa eneo hilo.
"Kama jinsi  mtaona katika Kliniki ya Mkoa wa Pwani  sijafukuza ama kumsimamisha mtendaji  wangu yeyote  hii ni kwa sababu hawajatajwa  kuingiza miguu na wananchi kuhusika katika  kashfa yoyote ya uuzaji ardhi.
Waziri Silaa ametoa maelekezo  kwa  Kamishna wa Ardhi Mkoa wa Pwani  kufuatilia kiutaalamu na kwa kina malalamiko yote yaliyotolewa na wananchi  huku ameahidi kuwa  atarudi tena Mkoani hapa ambapo ndipo atakuja kutoa maamuzi.
Akifafanua kuhusu maeneo yaliyovunjwa  mwezi Juni  katika  eneo la Mitamba lililopo Kata ya Pangani  Wilayani Kibaha Mjini amesema  kuwa maelezo ya eneo la Mitamba amelichukua jana Julai 3 ambapo tayari  amempa maelekezo  Kamishna  wa Ardhi Mkoa wa Pwani  pia
wataalamu wake watafuatilia kwa undani zaidi huku akisisitiza  kuwa  baada ya uvunjaji Wizara imepokea maelekezo kutoka kwa Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan  kutatua  migogoro yote  ya ardhi   kwa  amani  na weledi wa hali ya juu  ilikukwepa kuleta  taharuki kwa jamii ndiyo sababu  iliyopelekea kusitisha uvunjaji wa nyumba katika eneo la Mapinga.
Aidha Waziri Slaa amewapa pole  watu wote ambao walikua na shauku ya kuona akitoa maamuzi na kuwataka wawe na mioyo ya subira.
Wakati huohuo Waziri Silaa amempongeza Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu  kwa kuwa mstari wa  mbele katika kutatua migogoro  ya ardhi.
Akizungumza kuhusu  tuhuma za Viongozi  wa Halmashauri  hasa  katika Idara ya Ardhi Kibaha ambao wamekuwa wakitajwa  kuhusiana na shutuma mbalimbali za kutumia madaraka yao  kinyume na maadili ya kazi  zao , amesema apelekewe majina yao watachunguzwa na pindi watakapo bainika watachukuliwa hatua za kinidhamu kwa mujibu wa sheria.
Ametoa pongezi  kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge  kutokana na jitihada zake za  kutatua migogoro  ya ardhi ndani ya Mkoa wa Pwani   wakati huohuo amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Halima Okash kwa  kukutana na wananchi kuwasiliza  na kuyamaliza  kwa suluhu yenye tija matatizo  ya ardhi ndani ya Wilaya yake ambapo ameweza kuwakutanisha mlalamikaji na mlalamikiwa na kutatua migogoro  mingi kwa njia ya suluhu ikiwamo kukubaliana kupeana fidia kwa njia mbadala.
Naye Mbunge wa  Jimbo la  Bagamoyo  Mharami  Mkenge aliyekuwa katika eneo la Kliniki hiyo  amepongeza sana  jitihada zinazofanywa na Waziri Silaa amesema kwa upande wa Wilaya  ya Bagamoyo  wanatarajia baada ya kupata ufumbuzi wa migogoro  ndani ya Jimbo  hiyo Halmashauri  itakaa na kuipanga vyema  Mji huo wenye vivutio  lukuki vya asili.
Aidha Waziri  Silaa ameunda Mikoa  Mikoa miwili  lengo kumaliza migogoro  ya ardhi Mkoa wa Pwani.
Mhe. Silaa amesema Wizara yake imefikia maamuzi ya kuanzisha Mikoa miwili ya Ardhi katika Mkoa wa Pwani ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Dkt. Samia Suluhu Hassan  katika falsafa yake ya maridhiano, kujenga upya nchi, uvumilivu na mageuzi yaaani 4R
Waziri Silaa amesema hayo katika   Kliniki ya Ardhi Bagamoyo kwa ajili ya kusikiliza na mitatu kero za migogoro ya ardhi kwa wananchi iliyofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Majengo.
Aidha, Waziri Silaa amesema kuwa ofisi za Ardhi zinapaswa kutoa huduma kwa uwazi ili  wananchi waweze kusikilizwa pasipo kifucho.
Mikoa mipya iliyoanzishwa  ni Pwani Kaskazini itakayohusisha  Wiilaya ya Kibaha na Halmashauri ya Chalinze huku Kanda ya Kusini  ni Mkuranga,Kibiti,Kisarawe  na Mafia .






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...