MTEJA wa Bank of Africa Tanzania tawi la NDC jijini Dar es Salaam, Samira Ayubu Msangi, ambaye aliibuka mshindi wa pili wa zawadi katika droo ya pili ya kampeni ya Kigitali ijulikanayo kama “Ingia B-Mobile utoke na Iphone 15 inayoendeshwa na benki hiyo amekabidhiwa zawadi yake ya ushindi ya simu aina ya I-phone 15. Droo ya kumpata mshindi ilisimamiwa na Bodi ya Taifa ya Michezo ya Kubahatisha.
Kampeni ya “Ingia B-Mobile utoke na Iphone 15” ilianza Juni 10, 2024 na itaendeshwa kwa miezi 3 na wateja wengine wenye bahati wataweza kujishindia simu janja za kisasa aina ya I-phone 15. Ili kushiriki kampeni wateja wa Bank of Africa, wanatakiwa kufanya miamala ya kidigitali kupitia programu ya Benki ya simu ya kiganjani (B-Mobile) au kwa kupiga (*150*13#) kufanya miamala mingi iwezekanavyo na kutoa pesa kupitia WAKALA wa BOA ili kuingia kwenye droo inayofanyika kila mwezi.
Akiongea wakati wa droo hiyo,Mratibu wa bidhaa na huduma za kidigitali wa Bank of Africa, Fortunatus Joachim, alisema kampeni hii imelenga kuwezesha wateja wa Benki kutumia mfumo wa kidigitali kupata huduma za kibenki ambao umeboreshwa kutumia simu ya kiganjani kukidhi mahitaji yao.
“Kama benki tumedhamiria kutoa bidhaa na huduma bora zinazokidhi mahitaji ya wateja, benki itaendelea kukuza na kuleta mawazo mapya ya ubunifu kuendana na kasi ya ukuaji wa matumizi ya kidigitali katika tasnia ya benki kwa ajili ya kukuza zaidi ajenda jumuishi ya kifedha," alisema Fortunatus.
Nae, Mkuu wa Mawasiliano na Masoko, Nandi Mwiyombella, alisema : “Kupitia kampeni hii, wateja wetu na wapya wanaotumia huduma za benki mtandao (Mobile Banking) wataingia katika droo iwapo watafanya miamala kwa njia ya kidigitali na kutoa fedha angalau mara moja kutoka BOA WAKALA.
Kampeni hii ni kielelezo cha lengo la kimkakati la benki kuweka bidhaa na huduma zake katika mfumo wa kidijitali na hivyo kukuza ushirikishwaji wa kifedha pamoja na urahisi wa wateja kupata huduma za benki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...