Matukio mbalimbali Pichani yakimuonesha Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura akikagua gwaride na baadae akizungumza na maofisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali wa Mkoa wa Kilimanjaro Agosti 16,2024 ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi mkoani humo.
IGP Wambura amewataka maofisa, wakaguzi na askari kuendelea kutekeleza majukumu yao ya kazi za Polisi kwa kuzingatia nidhamu, weledi na uadilifu pamoja na kutenda haki kwa wananchi wanaowahudumia na kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa mteja wa Ndani na Nje sambamba na utekelezaji wa maelekezo ya Tume ya Haki Jinai.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...