Na Mwandishi wetu, Mirerani
VIONGOZI wa kamati za usuluhishi na usalama migodini kwenye machimbo ya madini ya Tanzanite kitalu B na D, Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wamepatikana baada ya kuchaguliwa na wachimbaji.
Ofisa madini mkazi Mirerani (RMO) Nchagwa Chacha Marwa, kamati ya ukuta unaozunguka migodi ya madini ya Tanzanite na Mwenyekiti wa chama cha wachimbaji madini mkoa wa Manyara (MAREMA) walisimamia uchaguzi huo uliofanyika ukumbi wa Kazamoyo Inn (kwa Luka).
Nchagwa akitangaza matokeo hayo amesema Barnabas Mallya, ambaye hakuwa na mpinzani amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa kamati ya usuluhishi na usalama kitalu D, kwa kupata kura 63.
Amesema Hamis Kim (Komando) ambaye pia hakuwa na mpinzani amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti kitalu D kwa kupata kura 53.
Amesema nafasi ya Katibu wa kitalu D iliyogombewa na watu wawili, amechaguliwa Omary Rajab kwa kupata kura 35 dhidi ya Niki Kikuyu aliyepata kura 25.
"Nafasi ya Katibu msaidizi wa kamati amechaguliwa Yasir Kiwanda (Mazimuzi) ambaye hakuwa na mpinzani kwa kupata kura 45," amesema Nchagwa.
Amewataja wajumbe watano wa kamati ya kitalu D ni George Kishe 48, Yohana Maula 55, Michael Raphael 40, Elibariki Kessy (Masho) 48 na Joel Kisivanichi 49.
Kwa upande wa kitalu B Nchagwa amemtangaza Charles Chilala kuwa Mwenyekiti wa kamati hiyo kwa kupata kura 91 dhidi ya Fred Mbwambo aliyepata kura 34.
Amesema Makamu Mwenyekiti wa kamati ya usuluhishi na usalama kitalu B amechaguliwa Zephania Joseph Mungaya kwa kura 92 dhidi ya Dan Star Ngunda aliyepata kura 29.
RMO amesema Abubakari Madiwa amechaguliwa kuwa katibu kwa kura 49 baada ya kuwashinda Shwaibu Mushi kura 39 na Peter Agusti Msafiri kura 39.
Amemtangaza Agripina Casian kuwa Katibu msaidizi kwa kupata kura 74 dhidi ya Willy Mmary aliyepata kura 48.
Amewataja wajumbe watano wa kamati ya kitalu B ni Christopher Mushi (119), Mosses Kalimbu (99) Yusuf Mnyoti Maraa (88) Sokoi Mollel (92) na Hassan Ally (71).
Mwenyekiti wa kamati ya usuluhishi na usalama kitalu D Barnabas Mallya akizungumza baada ya kuchaguliwa amewashukuru wachimbaji na kuwasihi wajumbe kuwa waadilifu.
Mwenyekiti wa kamati ya usuluhishi na usalama kitalu B, Charles Chilala amewashukuru wachimbaji kwa kumchagua na kuahidi kutenda haki kwani bado ni kijana ana nguvu za kuzama mgodini.
Mwenyekiti wa MAREMA, Justin Nyari amewapongeza viongozi wote waliochaguliwa na kuwataka wasimamie haki bila kuwa na upendeleo.
Katibu wa MAREMA Tawi la Mirerani, Rachel Njau amesema baada ya uchaguzi wa kamati hizo kitachofuata ni uchaguzi wa viongozi wa MAREMA Tawi la Mirerani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...