Sehemu ya mtambo wa kutengeneza Asali.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Ufugaji Nyuki  ya Igembensabo Farm Implements LTD na Chamwino Beekeepers Honey Processing Plant Mazari Taji akizungumza  Waandishi wa Habari kuhusiana na changamoto ya Ufugaji na Uuzaji wa Asali.


 Na Chalila Kibuda ,Dodoma 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Ufugaji Nyuki ya  Igembensabo farm implements LTD  na chamwino Beekeepers Honey Processing Plant  Mazari Taji amesema kuwa Soko la Asali limekuwa kubwa ndani na nje ya nchi hivyo kunahitajika jitihada zaidi za kuendelea kuvuna Asali kisasa.

Mazari aliyasema hayo katika kiwanda chake kilichopo ndani ya Maonesho ya Nane Nane Nzuguni Jijini Dodoma,amesema kuwa Mamlaka zinazohusika katika kutoa vibali kuwa na dawati moja kuondoka na msululu WA makaratasi ya kufuata kila Ofisi.

Amesema kuwa kuendelea na kuwepo na kufuata taratibu katika kila Ofisi kuna sababisha kuwepo kwa njia ya panya katika usafirishaji wa Asali katika soko la ndani.

Hata hivyo amesema kuwa katika Viwanja vya ndege mtu akiwa na galoni ya Lita tano apite tu kwani anakwenda kuitangaza nchi kwani vikwazo wanayopata abiria wanakwenda na asali nje ya nchi haileti Afya.

Aidha amesema kuwa bidhaa za mizinga zinatokana na mbao ambazo sio Mali asili ambapo baadhi ya Mamlaka kuwakamata kigezo kuwa ni mali asili.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa wakati wa usafirishaji wa Asali wanahitaji kupata namba ya Gari inayobeba asali hali hiyo kwa Wafugaji wadogo hawawezi kumudu katika umiliki wa Gari.

Amesema katika utendaji wa kampuni inawafindisha Wafugaji wa nyuki pamoja na kuwapa mizinga na wanauza katika kampuni hiyo wanatoa mirabaha kwa Wafugaji hao.

Hata hivyo amesema serikali imeweka mazingira mazuri katika Ufugaji wa nyuki hivyo Mamlaka kuangalia namna ya kuwasaidia na sio kuwadidimiza

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...