Kada wa Chama Cha Mapinduzi  Chikukupi Njelu Kasaka akizungumza na wananchi na Waandishi wa Habari mara baada ya kuchukua fomu ya kugombea ubunge wa wa Afrika Mashariki ndani ya Chama hicho ,Katika Ofisi Ndogo Lumumba Jijini Dar es Salaam.
Kada wa Chama Cha Mapinduzi  Chikukupi Njelu Kasaka akikabidhiwa fomu ya kugombea ubunge wa Afrika Mashariki  ndani ya Chama ,jijini Dar es Salaam.


Na Mwandishi Wetu
KADA wa Chama Cha Mapinduzi Chikukupi Njelu Kasaka amechukua fomu ya kugombea ubunge wa bunge la Afrika Mashariki (EALA) leo tarehe 14.08.2024. Kada huyo amechukua fomu katika ofisi ya Chama Cha Mapinduzi iliyopo jijini Dodoma akisindikizwa na makada mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi

Chikulupi Njelu Kasaka ambae kitaaluma ni Mwanasheria na Wakili, ni mbobezi wa masuala ya siasa, utawala na diplomasia mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 12 katika mahusiano ya kimataifa na diplomasia.

Chikulupi amekitumikia Chama Cha Mapinduzi katika nyanja tofauti na pia ni mjumbe katika kamati mbalimbali.

Baada ya kuchukua fomu hiyo Chikulupi Kasaka akiongea na waandishi wa habari ameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dr Samia Suluhu Hassan kwa juhudi mbalimbali anazofanya katika kukuza umoja na uchumi katika jumuia ya Afrika mashariki. Chikulupi ameahidi kuindeleza kazi hiyo ili kuiwezesha nchi yetu kupiga hatua kiuchumi kwa kuimarisha uchumi na fursa kwa vijana na taifa kwa ujumla.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...