MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu,akichangia Muswada wa Sheria ya Viwanja vya Ndege Tanzania wa Mwaka 2024 Bungeni jijini Dodoma.

.......

MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu amechangia Muswada wa Sheria ya Viwanja vya Ndege Tanzania wa Mwaka 2024 ,huku akigusia mambo mawili ambayo ni vyanzo vya Mapato vya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege(TAA),na usalama wa abiria na watumiaji wa viwanja vya ndege.

Akichangia muswada huo Bungeni Jijini Dodoma,Mtaturu ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu amesema kupitisha kwa Muswada huo kutawezesha kuwapa Mamlaka TAA na kuwatoa kwenye uwakala ili waweze kusimamia vizuri viwanja vya ndege.

Amesema kwam ujibu wa Mamlaka inayosimamia usalama wa anga Duniani(ICAO),ina vigezo vyake ambavyo inavitoa kila mahala,hivyo kama taasisi haina uwezo mkubwa wa kifedha haitaweza kuwa na ushindani katika viwanja vingine.

“Leo hii unaweza kutua uwanja wa ndege A ukaenda na uwanja wa ndege B utakuta ni tofauti sana kwa sababu ya huduma zilizopo pale ndani kwa hiyo tukiifanya hii mamlaka ikawa na uwezo wa fedha itaweza kuboresha vigezo kwa mujibu wa ICAO ,”.amesema.

Ameiomba serikali kupitia wizara zinazohusika ikiwemo Wizara ya Fedha kukaa na kuona namna itakavyowaachia TAA kukusanya tozo ya huduma ambayo inatolewa na abiria iweze kubaki katika taasisi ambayo inaenda kupewa mamlaka kamili.

Amesema hilo litaiwezesha TAA kuwa na fedha zake zenyewe bila ya kusubiri kupeleka maombi Hazina ili kupata fedha kwa ajili ya kutengeneza au kuboresha viwanja vya ndege.

“Mimi hapa nataka niombe pamoja na uwekezaji mkubwa uliofanywa katika viwanja vyetu lakini vinatakiwa kuendelea kutunzwa,hii customer service charge iweze kuachiwa watu wa TAA ili waweze kuwa na uwezo wa kukusanya na kutumia na hivyo kuendana na vigezo vya ICAO ambavyo kimsingi ni standard ya dunia nzima,

“Hatuwezi kujiweka kama kisiwa na kujikuta hatuboreshi viwanja vyetu,hii itafanya baadhi ya airlines isilete ndege katika viwanja vyetu hivyo tutakosa fursa kubwa ya kiuchumi na sasa hivi tumeboresha suala la utalii hivyo litakuwa limezuia watalii baadhi kuletwa nchini kwetu moja kwam oja,huu ni ushauri wetu kama kamati naamini serikali itaendelea kulifanyia kazi kuhakikisha inawapa TAA kukusanya fedha hizi,”.ameongeza.

Jambo la pili alilozungumzia ni usalama wa usafiri wa anga ambapo Mtaturu ameomba lipewe kipaumbele kwa sababu mtu akiwa salama anakuwa na uhakika na safari yake.

“Ombi langu ni kwamba ili kumpa comfort mtumiaji kwa maana ya abiria lazima tumuhakikishie usalama wake,kumekuwa na mgongano kwamba wenzetu wa TAA wana vifaa vya rescue kwa maana wana magari ya zima moto na vifaa vyake,kwa sasa hali ilivyo ina maana kwamba wewe kama una gari halafu dereva hakuhusu ina maana huna uhakika kama chombo chako kipo salama,

“Ombi letu ni kwamba wawe na kikosi cha zimamoto katika viwanja vya ndege ili iwe ni kitengo chao wenyewe waweze kuwa na mamlaka ya kusimamia wale wafanyakazi ambao ni askari wa zimamoto, lakini leo hii akitokea mfanyakazi amefanya makosa Wizara ya Uchukuzi haina mamlaka ya kumchukulia hatua yoyote kwa sababu sio mfanyakazi aliyemuajiri,”amesema.

Amesema ili usalama na usimamiz uwe mzuri ni vyema sasa serikali ifikirie kuwa na kikosi cha zimamoto maalum cha kuzuia majanga ya moto katika viwanja vya ndege kwak usimamiwa na TAA kupitia Wizara ya Uchukuzi tofauti na ilivyo sasa inasimamiwa na Mambo ya Ndani.

“Tukifanya hivyo tutawavutia airlines mbalimbali duniani ziweze kuleta ndege zao hapa kwak uwa usalama unakuwa mkubwa na kuufanya vivutio vikubwa ikiwemo kuendana na utaratibu wa sasa wa kuboresha masuala ya utalii duniani,’’.ameongeza.

PONGEZI KWA RAIS.

Amempongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya kusimamia serikali ya awamu ya sita lakini na kuiongoza nchi sawia ambapo Tanzania ipo salama kwa hakika wabunge na wananchi wanajivunia yeye kwa kazi anayoifanya.

“Ushahidi tosha tunauona sasa SGR watu waliyokuwa wanaizungumzia kama historia sasa Dar es salaam kuja Dodoma kwa saa 4,hili ni jambo kubwa na ilikuwa ndoto lakini sasa imetimia na hiyo ni dalili mojawapo ya uongozi thabiti alionao Rais wetu,

“Lakini katika majimbo yetu tumeona maendeleo makubwa wananchi wamefikiwa na huduma mbalimbali za kijamii,sisi tunajivunia katika uongozi wake maana tumeona mabadiliko ya kimaendeleo na kweli uungwana ni vitendo hivyo lazima tumpongeze na kumtia moyo sana Rais wetu kwamba watanzania wanamuunga mkono katika nyanja zote,”.amesema.

PONGEZI KWA SPIKA.

Amempongeza Spika Dkt Tulia Ackson kwa kazi kubwa anayoifanya ya kusimamia Bunge na kuwaomba watu wa Mbeya waendelee kuna na Imani nae na mwakani wampitishe ili arudi bungeni na kuendelea kuwaongoza.

“Jana baada ya kusimamia lile suala la mgogoro wa shamba la Malonje wananchi wengi wamepongeza namna ulivyosimamia haki ya wananchi wale na namna ulivyoelekeza kupitia kiti chako kuhakikisha wananchi wanaishi salama na kuhakikisha utengamano wa amani unapatikana,kwa hakika unaitendea haki nafasi hiyo na ndio maana ulipewa hata Urais wa mabunge duniani,

“Na wale watu wa Mbeya tunaendelea kuwaomba waendelee kuwa na imani na wewe na mwakani wakupitishe kwa mwendo wa mserereko ili urudi tena bungeni uendelee kutuongoza,”.ameeleza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...