Mwenyekiti wa Taasisi ya Mazingira  na Maliasili Tanzania Mwanawetu Saidi akifafanua  jambo mbele ya Waandishi wa habari hawapo pichani


Na Khadija Kalili Michuzi Tv 

TASISI isiyo ya kiserikali ambayo inajihusisha na utunzaji wa mazingira Mkoani Pwani  inayofahamika  kama Mazingira na Utalii  nayoongozwa na Mwanawetu Saidi wamefanya ziara katika shule za Muheza na Mount Calvary.

Akizungumza  na Waandishi  wa habari Mwanawetu amesema kuwa  wametembelea Shuleni  hapo ili kutoa elimu ya  kuhifadhi na kutunza  mazingira  kwa faida ya vizazi vijavyo.

"Tunasisitiza jamii kujiunga na klabu za  kutunza na kulinda  mazingira sambamba na kutumia nishati safi" amesema Mwanawetu.

Amesema kuwa Taasisi yao inajihusisha na kutoa elimu kwa jamii katika kutunza mazinga ya baharini na nchi kavu ikiwemo wanyama wa porini kwa ujumla.

Wakiwa Shuleni  hapo wamesisitiza matumizi ya  nishati safi  katika kupika chakula cha wanafunzi na kuacha kutumia mkaa na kuni. 

Muasisi wa Partnership for Green Future Rehema Peter  amesema kuwa  jukumu lao kubwa ni kutoa elimu ya utunzaji  mazingira  na safari yao imeanza kwa kutembelea  Shule ya msingi Muheza,Kibaha ambapo wamekuta kuna chagamoto za ukosefu wa matundu ya choo tunaendele kutafuta wadau ili shule zetu za msingi  ziwe na mazingira safi na  salama.

"Tusitumie  kuni wala mkaa katika  kumuunga mkono Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan  katika kutumia nishati safi. 

Akizungumza kwa niaba ya Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mount Calvary Eric Kilonzo amesema  wamefurahishwa na ugeni wa wanamazingira hao na wamepokea hamasa ya utunzaji mazingira na wameanza mchakato wa kuandaa majiko ambayo yatapika kwa kutumia nishati safi.

Mwisho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...