Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiagana na Wananchi wa Morogoro mara baada ya kuwahutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Jamhuri ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya Kikazi mkoani humo tarehe 06 Agosti, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipiga picha ‘selfie’ na wananchi wa Morogoro wakati akiondoka katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro mara baada ya kuwahutubia tarehe 06 Agosti, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwahutubia Wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Morogoro kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Jamhuri ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya Kikazi tarehe 06 Agosti, 2024.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Serikali imejipanga kurejesha ile hadhi ya kihistoria ya Mkoa wa Morogoro kuwa mkoa wa viwanda kwa kufufua viwanda na kuvutia uwekezaji mpya.


Rais Dkt. Samia ameyasema hayo wakati akihutubia wakazi wa Mkoa wa Morogoro katika Uwanja wa jamhuri akihitimisha ziara yake ya siku 5 kwenye Mkoa huo.


Aidha, Rais Dkt. Samia amesisitiza kuwa uwepo wa miundombinu ya reli na uwepo wa umeme wa uhakika kutoka Bwawa la Julius Nyerere unaufanya Mkoa wa Morogoro kuwa sehemu nzuri kwa uwekezaji.


Katika ziara yake Mkoani humo Rais Samia alitembelea uwekezaji wa upanuzi wa viwanda uliofanywa Mkoani humo ikiwemo Kiwanda cha Sukari cha Mtibwa, na Kiwanda cha Sukari cha Kilombero.


Pamoja na mambo mengine, Rais Samia amesema kuwa upanuzi huo wa uwekezaji kwenye viwanda unampa imani kuwa ifikapo mwaka 2025/2026 Tanzania itakuwa katika nafasi nzuri ya kujihakikishia uzalishaji wa sukari kukidhi mahitaji yake.

Rais Samia pia amesema kuwa uwezekaji huo na upanuzi wa viwanda vilivyopo ni ishara kuwa Tanzania ina mazingira bora na yanayovutia kwa uwekezaji wa viwanda. Hivyo, ametoa rai kwa wakulima kuendelea kuzalisha kwa wingi ili kulisha viwanda vinavyojengwa.

Mapema leo, Rais Samia alizindua Kiwanda cha Sigara cha Serengeti (SCC) katika eneo la Kiwanda cha Uchakataji Tumbaku cha Mkwawa (MTPL) ambapo amepongeza uwekezaji huo ambao utakamilika Juni 2025, na kuzalisha ajira mpya 12,000 Mkoani Morogoro.

Sharifa B. Nyanga
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu













Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...