RAIS  wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi atembelea banda la TADB katika Maonesho ya Saba ya Kilimo "Nane Nane" 2024, Dole Kizimbani – Unguja.

Rais Mwinyi ametembelea banda hilo alipokuwa akifungua rasmi maonesho ya saba ya Kilimo (nane nane) Zanzibar tarehe 3/8/2024.

Katika banda la TADB Mhe. Dkt. Mwinyi amepokelewa na Kaimu Meneja wa Kanda ya Zanzibar, Bw. Michael Madundo na kupatiwa muhtasari wa maendeleo ya benki ikiwemo taarifa ya utolewaji wa mikopo, idadi ya wanufaika wa mikopo ya benki Zanzibar pamoja na:

✅️ Jitihada zinazofanywa na benki katika kutoa elimu ya fedha na kilimo biashara Zanzibar

✅️ Mendeleo ya Mradi Shirikishi wa Wasindikaji, Wazalishaji wa Maziwa Tanzania (TI3P) ndani ya Zanzibar

✅️ Maendeleo ya Mfuko wa Dhamana wa Wakulima Wadogo (SCGS)

🟢 Mhe. Dkt. Mwinyi pia alipata nafasi ya kuona kazi za wanufaika wa TADB ikiwemo Kampuni ya Bin Mwewe wakulima wa Matunda na mbogamboga, Shemsa Taraba na Kampuni ya MPF wafugaji wa kuku wa mayai.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...