Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi, amewasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ngurah Rai Bali, Indonesia kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Pili wa Jukwaa la Indonesia na Afrika pamoja na Mkutano wa Viongozi kujadili ubia wa Maendeleo unaoanza kesho tarehe: 1 hadi 3 Septemba 2024.
Rais Dk. Mwinyi na ujumbe wake walipokelewa na Naibu Waziri wa Biashara wa nchi hiyo, Dkt. Jerry Sambuaga, pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Indonesia, Ndugu. Makocha Tembele.
Rais Dk. Mwinyi ameambatana na mkewe, Mama Mariam Mwinyi, akiwa nchini Indonesia, atafanya pia ziara ya kikazi ambayo itaanzia Bali na kumalizia jijini Jakarta.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...