Afisa Maadili, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bi. Modesta Mtui akitoa elimu ya maadili kwa Mkurugenzi wa bidhaa za Asas Bw. Ahmed ASAS (kulia) katika maonesho ya sikukuku ya wakulima (Nanenane) yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma, tarehe 7 Agosti, 2024.
Afisa maadili kutoka Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bi. Modesta Mtui (kushoto) akitoa maelezo kuhusu Mfumo wa Ujazaji wa Matamko ya rasilimali na madeni ya viongozi wa umma kwa njia ya mtandao kwa Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mhe. Remidius Mwema (kulia) katika maonesho ya sikukuku ya wakulima (Nanenane) yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma, tarehe 7 Agosti, 2024.
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mhe. Jaji (Mst.) Methew Mwaimu akiongea na maafisa wa SEkretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma tarehe 7.8.2024 alipotembelea banda la Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma katika maonesho ya kilimo ya Nane Nane yanayoendelea Nzuguni Jijini Dodoma.
Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji (Mst.) Sivangilwa Mwangesi akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa klabu ya Maadili kutoka shule ya Sekondari ya Nkonze pamoja na walimu wao walipotembelea banda la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma katika maonesho ya wakulima Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma, tarehe 7 Agosti, 2024.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bi. Teddy Njau (wa kwanza kushoto) akitoa maelezo kwa Katibu wa Bunge Bi. Nenewa Mwihambi (kulia mwenye nguo nyekundu) tarehe 7 . 8. 2024 alipotembelea banda la Sekretarieti ya Maadili katika maonesho ya kilimo ya Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...