Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Jumanne Sagini akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa saba wa mwaka wa Taasisi ya Utatuzi wa Migogoro ya Kibiashara (TIArb), unaoendelea kufanyika jijini Dar es Salaam leo Agosti 23, 2024.
SERIKALI imesema kuwa inaridhishwa kwa kiwango kazi inayofanywa na wasuluhishi wa migogoro, kwa sababu uzoefu unaonesha kwamba mashauri mengi ya kimigogoro ya kimikataba ya uwekezaji na katika sekta ya ujenzi.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Jumanne Sagini wakati wa mkutano mkuu wa saba wa mwaka wa Taasisi ya Utatuzi wa Migogoro ya Kibiashara (TIArb), unaoendelea kufanyika jijini Dar es Salaam leo Agosti 23, 2024.
Amesema kuwa Mashauri yanapokwenda mahakamani inachukua muda mrefu kukamilishwa lakini wanapokutana na kuzungumza chini ya watu waliobobea katika usuluhishi wakafikia mwafaka kwa muda mfupi na inapelekea miradi kuendelea kutekelezwa na baada ya usuluhishi kila upande unatoka bila manung'uniko moyoni.
"Lakini ukienda kwenye usuluhishi mara nyingi migogoro huchukua muda mfupi kutatuliwa." Amesema Sagini
Akizungumzia sera zilizopo, Sagini amesema sera ipo bayana kwa sasa wameshasajili taasisi za usuluhishi wa migogoro saba.
"Zimesajiliwa hapa nchini na zinatambuliwa na wizara ya katiba na sheria ambapo taasisi hizo zinahusika moja kwa moja katika usuluhishi wa migogoro mbalimbali inayotokea kibishara, Ujenzi na katika miradi mbalimbali ya uwekezaji wa kimtaifa." Ameeleza
Amesema kuwa hata upande wa Mahakama, Jaji mkuu anasisitiza kwenda kwenye usuluhishi wa migogoro nje ya Mahakama katika kutafuta njia mbadala za kumaliza migogoro bila kufika Mahakama.
"Kutokana na Ukuaji wa sekta ya Ujenzi na Uwekezaji wa kimataifa hapa nchini Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pia alisisitiza uwepo wa taassisi hizo ili inapotokea migogoro iweze kutatuliwa kwa mazungumzo kuliko kufika Mahakamani.
Kwa Upande wa Raisi wa TIArb, Adv. Madeline Kimei, akizungumza wakati wa mkutano huo amesema kuwa mwaka huu mkutano huo umejikita katika kuangazia masuala ya ujenzi na Uwekezaji wa kimtaifa.
Kwa Upande wa Katibu wa TIArb, Usaje Mwambene amesema taasisi hiyo inapokea migogoro kwa lengo la kusuluhisha nje ya mfumo wa Mahakama ambapo imezoeleka kuwa inapotokea lazima kuipeleka mahakamani ndipo waweze kupata suluhu.
"Taasisi hii imeanzishwa kwa lengo la kuwawezesha wadau wenye migogoro kuweza kuisuluhisha migogoro yao nje ya mfumo wa kimahakama." Amesema
Mkutano huo ulikuwa wa siku mbili, kwa jana walijikita katika kuangalia migogoro katika sekta ya Ujenzi na leo wanaaangalia namna ya usuluhishi wa migogoro katika Uwekezaji wa kimataifa.
Mkutano huo umekutanisha wadau wa ndani na nje ya nchi kwa lengo la kushirikiana, kujengeana uwezo na kupeana uzoefu wa namna ya kusuluhisha migogoro ya sekta ya ujenzi, Uwekezaji wa kimataifa pamoja na kibiashara.
Upande wa Katibu wa TIArb, Usaje Mwambene akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa saba wa mwaka wa Taasisi ya Utatuzi wa Migogoro ya Kibiashara (TIArb), unaoendelea kufanyika jijini Dar es Salaam leo Agosti 23, 2024.
Baadhi ya wadau wa Usuluhishi wa migogoro wakiwa katika Mkutano Mkuu wa Mwaka.
Picha ya pamoja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...