WACHEZAJI 100 wameshiriki mashindano ya siku moja ya 'KCB East Afrika Golf Tour' ambayo yamefanyika katika viwanja vya Lugalo gofu Kawe jijini Dar es Salaam.
Mashindano hayo yameshirikisha klabu zote nchini wakiwemo watoto (juniors) nchini na wachezaji kutoka nchi za Uganda, Rwanda, Kenya na Burundi.
Akizungumza na Wanahabari Leo Agosti 03,2024 Jijini Dar es Salaam Mkuu wa Utendaji Kivita na Mafunzo, Meja Jenerali Ibrahim Mhona amewapongeza benki ya KCB kwa kuchukua hatua ya kushirikisha watoto katika shindano hilo.
Mhona amesema mchezo wa gofu haujapiga hatua sana hapa nchini, lakini klabu ya Lugalo inapiga hatua kuhakikisha inaanda timu ya siku zijazo.
"Pongezi kwa watoto ambao wamefanya vizuri na kupatiwa zawadi zao, wachezaji wasiofanya vyema wakati ujao watafanya vizuri katika mashindano mengine.
Mhona amewapongeza wazazi kwa kuwaruhusu watoto kucheza mchezo wa gofu ambao unafanya vizuri Tanzania na Afrika Mashariki na Kati.
Naye, Nahodha wa watoto (Juniors), Ally Kayombo amewaomba Makampuni mengine kujitokeza kudhamini mashindano ya watoto kwa lengo la kuendelea vipaji vyao.
"Ombi letu kwa makampuni mengine kama KCB kujitokeza kudhamini mashindano kama ili watoto washirikii au kuandaa mashindano ya vijana."
Nahodha huyo amesema mashindano ya awamu hii wameboresha zawadi tofauti na miaka iliyopita, inaongeza chachu ya kuongeza bidii.
Katika mashindano hayo katika kiwanja cha 18 mshindi kwanza wa Hafidhi Twalibu ameshinda pointi 46 wakati nafasi ya pili Ni Stanley Emilias amepata pointi 45 huku Sabrina Juma akiwa mshindi wa tatu akipata pointi 22.
Wengine ambao wamecheza viwanja tisa upande wa close mshindi wa kwanza, Frank Emmanuel pointi 49 wa pili Joseph Msaada amepiga pointi 50 huku nafasi ya tatu ni Ellah Muga ameshinda pointi 68.
Mkuu wa Utendaji Kivita na Mafunzo JWTZ Meja Jenerali Ibrahim Mhona akipiga Mpira kwenye eneo la kuanzia Mchezo wa Gofu (Tbox) Kwenye shindano la KCB East Africa Golf Tour linalofanyika Kwa siku Moja Katika Klabu ya Gofu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ Lugalo.
Kushoto Mkurugenzi wa Benki ya KCB Cosmos Kimario akadhalika zawadi Kwa Mshindi wa Kwanza upande wakike kwa washiriki watoto (juniors) katika shindano la KCB East Afrika gofu tour,kulia kwake Mkuu wa Utendaji Kivita na Mafunzo JWTZ Meja Jenerali Ibrahim Mhona Leo Agosti 03,2024 Viwanja vya Klabu ya Lugalo gofu Jijini Dar es Salaam
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...