Mkuu wa Sehemu ya Maendeleo ya  Mkonge wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB), Simon Kibasa akizungumza na wananchi Waliotembelea Banda la Bodi ya Mkonge Katika Maonesho ya Kilimo Kitaifa Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.
Mkuu wa Sehemu ya Maendeleo ya  Mkonge wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB), Simon Kibasa akionesha wananchi bidhaa zinazotokana na zao la Mkonge wakati Waliotembelea Banda hilo kwenye Maonesho ya Kilimo Kitaifa Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.


*Ya pili kwa uzalishaji Duniani
Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv 
TANZANIA inaongoza kwa ubora wa Mkonge duniani na kuwa nchi ya pili kwa uzalishaji wa zao hilo duniani ambapo imezalisha tani 56,000 kwa kipindi cha mwaka 2023.

Akizungumza katika katika Maonesho ya Kilimo Kitaifa Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma, Mkuu wa Sehemu ya Maendeleo ya Mkonge wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB), Simon Kibasa amesema mahitaji ya Mkonge duniani makubwa ikilinganishwa na kiasi kinachozalishwa.

Amesema Brazil ni nchi ya kwanza kwa uzalishaji lakini Tanzania inaipita kwa ubora kutokana na kuwa na mitambo ya kisasa katika kuchakata mkonge.

"Uzalishaji wa Mkonge upo katika mikoa 16 ambapo Bodi inaendelea kuhamasisha wananchi kuingia katika kilimo hicho kutokana na kuwepo kwa soko kubwa katika soko la Dunia.

"Mahitaji ya soko la mkonge ni tani Milioni mbili ambapo wananchi wakiingia katika kilimo hicho Tanzania itaongoza kwa uzalishaji na ubora zaidi ya sasa," amesema.

Aidha kiwango cha uzalishaji duniani 600,000 hivyo kunafanya soko hilo kuelemewa hatuaà yanayotokana mahitaji kuwa makubwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...