Meneja wa Bank of Africa Tanzania Tawi la Arusha Francis Mizambwa, akimkabidhi zawadi ya simu mshindi wa droo ya tatu ya kampeni ya kidijitali ya BOA Innocent Boniphace Kisole katika hafla fupi iliyofanyika tawi la Arusha .
Na Mwandishi Wetu
MTEJA wa Bank of Africa Tanzania, Innocent Kisole ameibuka mshindi wa I-phone 15 Pro katika droo ya mwisho ya bahati nasibu ya kampeni ya kidijitali “Ingia B-Mobile utoke na Iphone 15 Pro” iliyoendeshwa na benki hiyo hivi karibuni.
Bahati nasibu hiyo imefanyika katika ofisi kuu ya BOA benki, mbele ya Mkaguzi Mwandamizi wa Michezo ya Kubahatisha kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Irene Kawili. Kampeni ya Ingia B-Mobile utoke na Iphone 15 Pro ilianza tarehe 11 Juni 2024 na imedumu kwa miezi 3.
Akiongea wakati wa kuchezesha droo hiyo, Mratibu wa Bidhaa na huduma za kidijitali wa BOA benki Fortunatus Joachim amesema “ wakati kampeni inaelekea ukingoni tunafurahishwa na ushirikishwaji na msisimko ambao kampeni hiyo imeleta kwa wateja wetu ambayo mafanikio yake yameonekana mazuri kupitia ukuaji wa mapato”.
Naye Mkuu wa Mawasiliano na Masoko na Mawasiliano Nandi Mwiyombella aliongeza kuwa benki hiyo inatarajia kuendelea na kampeni na shughuli shirikishi zaidi zitakazopelekea mwingiliano zaidi wa bidhaa na huduma za benki hiyo na zawadi za kusisimua zitatolewa.
Kampeni hii ni kielelezo cha lengo la kimkakati la Benki kuweka bidhaa na huduma zake katika mfumo wa kidijitali na hivyo kukuza ushirikishwaji wa kifedha pamoja na urahisi wa wateja kupata huduma za
benki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...