Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara, NBC Premiere League jana iliipamba mechi kati ya Azam FC na Simba SC maarufu kama ‘Mzizima Derby’ kwa kuandaa matukio kadhaa ikiwemo kukabidhi zawadi ya tuzo na pesa taslimu kwa mchezaji na kocha bora wa ligi hiyo kwa mwezi Agosti.

Mechi hiyo ilifanyika kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar na kuisha kwa timu ya Simba SC kuibuka na ushindi wa goli 2-0. Wateja mbalimbali wa benki ya NBC walipata fursa ya kuutazama mchezo huo wakiwa katika jukwaa la VIP kupitia udhamini wa benki hiyo.

Meneja wa Benki ya NBC tawi la Zanzibar Bw Abdul Karim Mkila aliiwakilisha benki hiyo katika kukabidhi tuzo na hundi ya fedha yenye thamani ya sh milioni moja, kwa mchezaji bora mwezi Agosti, ambae ni kiungo wa Simba SC, Jean Charles Ahoua huku Mwenyekiti wa Chama Cha Soka Mkoa wa Dar Es Salaam (DRFA) Lameck Nyambaya akikabidhi zawadi kama hizo kwa kocha mkuu wa klabu ya SC Fadlu Davids ambae aliiibuka kocha bora kwa mwezi huo.

Katika mchezo huo wa jana ilishuhudiwa kipa wa Simba SC, Moussa Camara akiibuka mchezaji bora wa mchezo huo na kukabidhiwa zawadi ya tuzo kutoka benki hiyo.


Meneja wa Benki ya NBC tawi la Zanzibar Bw Abdul Karim Mkila (Kushoto) akikabidhi hundi yenye thamani ya sh milioni moja kwa kiungo wa Simba SC, Jean Charles Ahoua aliyetangazwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya NBC kwa mwezi Agosti wakati wa mechi kati ya Azam FC na Simba SC  iliyofanyika kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar jana. Klabu ya Simba SC iliibuka na ushindi wa goli 2-0.



Mwenyekiti wa Chama Cha Soka Mkoa wa Dar Es Salaam (DRFA) Lameck Nyambaya (Kushoto) akikabidhi tuzo kwa kocha mkuu wa klabu ya SC Fadlu Davids alietangazwa kocha wa Ligi Kuu ya NBC kwa mwezi Agosti wakati wa mechi kati ya Azam FC na Simba SC  iliyofanyika kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar jana. Klabu ya Simba SC iliibuka na ushindi wa goli 2-0,



Mwenyekiti wa Chama Cha Soka Mkoa wa Dar Es Salaam (DRFA) Lameck Nyambaya (Kushoto) akikabidhi hundi yenye thamani ya sh milioni moja  kwa kocha mkuu wa klabu ya SC Fadlu Davids alietangazwa kocha Bora wa Ligi Kuu ya NBC kwa mwezi Agosti wakati wa mechi kati ya Azam FC na Simba SC iliyofanyika kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar jana. Klabu ya Simba SC iliibuka na ushindi wa goli 2-0,



Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa Benki ya NBC tawi la Zanzibar Obedy Ngavatula (Kulia) akikabidhi tuzo ya mchezaji bora kwa kipa wa Simba SC, Moussa Camara aliyeibuka mchezaji bora wa mchezo kati ya Azam FC na Simba SC uliofanyika kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar jana. Klabu ya Simba SC iliibuka na ushindi wa goli 2-0.



Kipa wa Simba SC, Moussa Camara akifurahia na tuzo yake baada ya kuibuka  mchezaji bora wa mchezo kati ya Azam FC na Simba SC uliofanyika kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar jana. Klabu ya Simba SC iliibuka na ushindi wa goli 2-0,



Meneja wa Benki ya NBC tawi la Zanzibar Bw Abdul Karim Mkila (Kushoto) akikabidhi tuzo kwa kiungo wa Simba SC, Jean Charles Ahoua aliyetangazwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya NBC kwa mwezi Agosti wakati wa mechi kati ya Azam FC na Simba SC  iliyofanyika kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar jana. Klabu ya Simba SC iliibuka na ushindi wa goli 2-0,







Katika mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar jana Klabu ya Simba SC  iliibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Azam FC

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...