Naibu Waziri Mkuu Dkt. Dotto Biteko (kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Alaf Limited Tanzania, Hawa Bayumi (kulia) wakati wa ufunguzi wa Maonyesho ya Kimataifa ya Viwanda (TIMEXPO 2024) yanayoendelea katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu, Michuzi tv
NAIBU Naibu Waziri Mkuu Mh. Dk Dotto Biteko ameelezea kuridhishwa na huduma na bidhaa za Alaf Limited Tanzania na kuitaka kampuni hiyo iendelee kuzingatia ubora.
Mh. Biteko aliyasema hayo Jumatano wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo katika Maonyesho ya Kimataifa ya Viwanda (TIMEEXPO 2024) aliyoyafungua rasmi katika Viwanja vya Sabasaba.
"Nawapongeza sana kwa kazi nzuri mnayofanya na pia Kwa kushiriki katika Maonyesho hata makubwa," alisema.
Mh. Biteko pia alihitaji kufahamu ikiwa suala la umeme kiwandani hapo lilishashugulikiwa baada ya kuwepo na malalamiko ya kukatikakatika kwa umeme mara Kwa mara, jambo ambalo lilikuwa linaathiri uzalishaji.
"Mheshimiwa tunakushukuru mno maana suala hili limeshashugulikiwa na sasa uzalishaji unaendelea vizuri,"alijibu Bi. Hawa Bayumi ambaye ni Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Alaf.
Meneja huyo aliipongeza serikali kwa kuhakikisha kuwa mazingira ya uzalishaji na biashara kwa ujumla ni mazuri.
"Tunatoa wito kwa serikali iendelee kuboresha mazingira haya zaidi ikiwemo kuangalia sera ambazo sio rafiki kwa wazalishaji na pia kuweka miundombinu sawa ikiwemo barabara ili usafirishaji uwe rahisi," alimueleza Naibu Waziri Mkuu.
Alieleza kuwa Alaf itaendelea kutoa suluhisho sahihi ya ujenzi kwa ujumla ikiwemo kuja na teknolojia mpya kama inayotumika kujenga maghala ya nafaka Mkoani Ruvuma ambayo imezingatia ubora wa hali ya juu na ni mpya kabisa.
ALAF ni moja ya makampuni yanayoshiriki katika TIMEXPO 2024 yaliyoanza Septemba 26 na yatamalizika Oktoba 2, 2024.
Maonyesho hata yameandaliwa na CTI Kwa kushirikiana na TANTRADE.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...