*Bilioni 38 zaongezwa kuondoa ukata kwa wanafunzi kutoka 200,000 hadi 530,000
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
Serikali kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu Juu (HESLB) kwa mwaka wa masomo 2024/2025 imetanga Shilingi bilioni 787 Kwa ajili ya jumla ya wanafunzi 245,799.
Hayo ameyasema Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo Dkt.Bill Kiwia wakati akitangaza orodha ya awamu ya kwanza kwa wanafunzi wataopata mikopo ya elimu ya juu kwa waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika katika Ofisi ya Bodi jijini Dar es Salaam.
Dkt.Kiwia amesema kuwa katika awamu ya kwanza wanafunzi 21,509 wanufaika mikopo hiyo na kuendelea na awamu nyingine.
Amesema kuwa Kwa mwaka huu,serikali bajeti hiyo wakiwemo zaidi ya wanafunzi 88,000 wa mwaka wa kwanza waliotengewa bilioni 284.8 ambayo bajeti hiyo ya mwaka 2024/2025 imeongezeka kwa shilingi bilioni 38 sawa na asilimia tano (5) ikilinganishwa na bajeti ya 2023/2024 ya bilioni 749 ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu.
Dkt. Kiwia amesema orodha hiyo ya awamu ya kwanza inajumuisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliopangiwa mikopo ya shahada ya awali,Shule ya Sheria Kwa vitendo na shahada ya uzamili.
Amesema orodha hiyo ya awamu ya kwanza wanafunzi 21,509 wataanza kupatiwa mikopo ambapo jumla ya shilingi za kitanzania bilioni 70.78 zinatumika.
"Leo tumeanza kutoa taarifa za mikopo kwa makundi yote,waliopangiwa mikopo,wapo ambao bado tunaendelea kufanyia kazi maombi yao na kila mwombaji atapata taarifa yake kwenye akaunti yake ile ile aloyotumia kuombea mikopo,na Wala hauhitaji kufika ofisi za HESLB"amesema Dkt Kiwia huku akisisitiza kuwa upangaji wa mikopo kwa wanafunzi wa stashahada na shahada ya uzamivu unaendelea.
Aidha Dkt Kiwia amesema kuwa bodi hiyo imeanza kuandaa malipo ya wanafunzi wapya na wanaoendelea na masomo ambao ni wanufaika wa mikopo,lengo likiwa ni kuhakikisha fedha zinafika vyuoni Kwa wakati huku akivitaka vyuo kuwasilisha matokeo ya mitihani ya wanafunzi wanaonufaika na mikopo wanaoendelea na masomo ili malipo yao yaandaliwe Kwa wakati bila kicheleweshwa.
"Kuna vyuo vichache,ambavyo bado havijawasilisha matokeo,tumewakumbusha na kuwasisitiza waharakishe kuwasilisha matokeo ya mitihani ya wanufaika ili na sisi tukamilishe malipo ya wanafunzi waliofaulu kuendelea na masomo"amesema Dkt Kiwia.
Amesema wanafunzi waliopangiwa kupata mikopo watapata taarifa kupitia simu zao za mikononi 'simu janja' au kompyuta kupitia akaunti zao walizoombea mikopo zijulikanazo kama 'SIPA'- Student's Individual Permanent Account.
Hata hivyo Dkt Kiwia amesema kuwa kupitia elimu waliyoitoa katika Shule za Msingi na sekondari Mikoa yote 31 kuhusu namna ya kuomba mikopo imesaidia kupunguza makosa Kwa waombaji kwani hapo awali kulikuwa na changamoto kubwa Kwa waombaji kukosea kuomba Jambo lililochelewesha mchakato na kuongeza kuwa Kwa mwaka wa masomo 2024/2025 wanufaika wa Mikopo pia watanufaika na ongezeko la mikopo hasa katika ada vyuoni.
Kwa upande wake Rais wa jumuiya ya wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu na vya Kati,TAHLISO Bi Zainab Kitima ameishukuru serikali chini ya usimamizi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kutoka shilingi 200,000 hadi 530,000 kwa kusema kuwa Sasa ongezeko hilo litapunguza mzigo Kwa wazazi na wanafunzi hasa wanaotokea kwenye familia zenye hali duni.
"Tunaishukuru sana serikali Leo kupitia HESLB tumesikia Mkurugenzi Dkt Kiwia akisema kuwa mikopo itafikishwa vyuoni Kwa wakati,ni taarifa njema sana Kwa wanufaika wa Mikopo ya elimu ya juu kote nchini"amesema.
Orodha ya awamu ya pili ya wanafunzi waliopangiwa mikopo Kwa mwaka wa masomo 2024/2025 inatarajiwa kutangazwa wiki ijayo na bodi hiyo ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu (HESLB).
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Dkt.Bill Kiwia akuzungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza orodha ya awamu ya kwanza ya wanafunzi wataonufaika mikopo ya masomo kwa mwaka wa masomo 2024/2025 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Dkt.Bill Kiwi And (mwenye suti) akiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa bodi hiyo pamoja Rais wa TAHLISO Zainab Kitima
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...