Na Khadija Kalili Michuzi Tv
MKUU wa Majeshi nchini Jenerali Jacob Mkunda (CDF) kupitia uratibu wa Baraza la Michezo la Majeshi ya Ulinzi Dunia Conseil International du Sports Military imewaleta wakufunzi na wataalamu kutoa mafunzo kwa makocha nchini ikiwa na lengo la kuwaaendeleza Maafisa wa Jeshi na Askari wenye taaluma ya michezo.
"Mafunzo haya yataimarisha mahusiano mazuri kati ya Tanzania na nchi ya Uholanzi (Netherlands)".
"Dhamira ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Tanzania ni kupata waalimu wazuri watakao saidia timu za JWTZ zinazoshiriki katika ligi mbalimbali nchini na kimataifa.
Hayo yamesemwa leo 11,Septemba,
2024 Kocha Rajab Bwamkuu kutika JWTZ alipozungumza na Waandishi wa Habari kwenye Uwanja wa JKT Mbweni uliopo Jijini Dar es Salaam.
Kocha Rajab Bwamkuu amezungumza kwa niaba ya wenzake amesema wanatoa shukran kwa Mkuu wa Majeshi CDF Jacob Mkunda kwa kuona umuhimu wa kuwaleta wakufunzi hao ambapo mbali na wakufunzi hao kutoka nje pia Shirikisho la Soka nchini (TFF) wamekuwa wakitoa mafunzo mbalimbali.
"Waalimu hawa wakigeni wapo mbali kimafunzo na wanavifaa vya kisasa hivyo tanatoa ahadi ya kufanya vizuri katika kuhakikisha timu za Majeshi na Taifa zinafanya vizuri" amesema Kocha Bwamkuu.
Aidha Bwamkuu ametaja majina ya Wakufunzi hao kutoka nchini Uholanzi (Netherlands) ni Rob Van Belkom,
Hans Feensta na Sigi Careera.
"Mafunzo haya ni ya wiki mbili na ijumaa jioni yatafungwa rasmi hii inatokana na mahusiano mazuri ya Chama Cha Mpira wa miguu Cha majeshi" amesema Bwamkuu .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...