MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Alhaj Othman Masoud Othman, Leo Jumamosi Septemba 21, 2024, amejumuika, pamoja na Masheikh, Waumini wa Kiislamu na Wananchi mbali mbali, katika Maziko ya Bi. Kesi Wakili Jaha, huko Mombasa SOS, Mkoa wa Mjini-Magharibi, Unguja.
Marehemu Bi. Kesi ambaye ni Mama Mzazi wa Mmoja wa Wasaidizi wa Mheshimiwa Makamu wa Kwanza wa Rais, alifariki-dunia, Jana Septemba 20, Nyumbani kwake, hapo hapo Mombasa, baada ya kuugua kwa kitambo.
Marehemu amesaliwa katika Masjid Jumaa, Msikiti uliopo Mombasa SOS (Kwa Baramia), ambapo Sala imeongozwa na Sheikh Profesa Hamed Rashid Hikmany, na kisha kuzikwa Kijijini kwao Kizimkazi Dimbani, Mkoa wa Kusini Unguja.
Mwenyezi Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Mahala Pema Peponi, Amiin!
Innalillahi Waina Ilayhi Raajiun!
Kitengo cha Habari,
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,
Septemba 21, 2024.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...