Washiriki wa kozi ya OCR official level 1 wakiwa katika Hifadhi ya msitu wa pande kama sehemu ya 'adventure' ya mchezo huo
Washiriki wa kozi ya OCR official wakipata mafunzo ya Adventure racing katika Msitu pande jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa kozi ya OCR official wakipata mafunzo ya Adventure racing katika Msitu pande jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV
TANZANIA ipo mbioni kuanzisha aina mpya ya mchezo ujulikanao kama Adventure Racing ambapo zaidi ya wanamichezo 50 wameshiriki mafunzo ya ukocha ya Level 1 kwa ajili kujifunza sheria na kanunu za mchezo huo.
Lakini pia lengo la mafunzo hayo ni kuwaandaa kuja kutoa mafunzo ikiwemo mashuleni ili kupata wachezaji kwa ajili ya michuano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa..
Akizungumza wakati wa siku ya kwanza ya mafunzo ya siku tatu jijini Dar es Salaam, mratibu wa mafunzo hayo Abdallah Juma Chapa kutoka Scope Event amesema Adventure Racing ni miongoni mwa michezo maarufu duniani, ukiwa ni mmoja wa michezo inayoshindaniwa katika michezo ya Olimpiki.
Lakini kwa hapa nchini Tanzania, mchezo huu bado ni mgeni na ndio maana wameanza kutoka mafunzo kwa walimu ili wafahamu sheria na taratibu za mashindano za mchezo huo ili watoke mafunzo kwa wachezaji.
Akiueleze mchezo huo, amesema Racing Adventure ni mchezo unaofanana na riadha, ndani yake ukiwa na michezo mingine yenye vikwazo mbalimbali ambapo mchezaji inabidi atumie maarifa ya ziada ili aweze kushinda.
Lakini pia amesema mchezo huu unaweza kuchezwa sehemu mbalimbali yakiwemo maeneo ya utalii na ni moja ya michezo inayopendwa duniani.
“Mwaka jana mchezo huu ulichezwa na watalii katika Mlima Kilimanjaro na kuvutia watu wengi sana,”
“Hivyo, tukaona haja ya kuanzisha mchezo huu hapa nchini na kualika wachezaji na makocha kutoka michezo mbalimbali kuja kushiriki semina hii kwa sababu kwa sehemu kubwa mchezo huu unafanana na riadha,”
Amesema kuwa ili kuanzisha mchezo huo hapa nchini Shirikisho la Dunia limeitaka Tanzania kuandaa kwanza mafunzo ili kuwapata walimu na baadae kusajili chama kwa ajili kuusimamia mchezo huo ili kupata uhalali wa kushiriki michuano mbalimbali duniani,” amesema Chapa.
Mafunzo hayo yametolewa na mtaalamu Nayibe Statia kutoka visiwa vya Carribean ambaye amesema kuwa anatamani kuiona Tanzania katika ramani ya dunia kupitia mchezo huu.
“Nimefurah sana kuja Tanzania, nchi ninayoipenda sana kwa ajili ya kutoa mafunzo haya,”
“Pia nimefurahi kuona utayari wa washiriki na shauku kubwa ya kuwa sehemu ya mchezo huu,” amesema.
Amesema kwa Afrika, mchezo huu unachezwa zaidi na Nigeria na Rwanda na Tanzania muda sio mrefu itakuwa miongoni kwa nchi hizo.
Pia amesema kuwa amekuwa akitoa mafunzo ya mchezo huo kwa nchi mbalimbali kwa njia ya mtandao ili kuutangaza zaidi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...