MHANDISI KIRITA AULA RUWASA
Na Mwandishi wetu, Babati
ALIYEKUWA  Meneja wa mamlaka ya maji na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) Mkoa wa Manyara, Wolta Kirita ameteuliwa kuwa kaimu mkurugenzi wa usambazaji maji na usafi wa mazingira RUWASA makao makuu.


Mhandisi Kirita anajaza nafasi iliyoachwa wazi na mhandisi Mkama Bwire aliyeteuliwa hivi karibuni kuwa kaimu mkurugenzi wa DAWASA.


Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na meneja uhusiano na masoko wa RUWASA, Athumani Shariff uteuzi huo unaanza mara moja.


Taarifa hiyo imeeleza kuwa Ruwasa imefanya mabadiliko madogo ngazi ya makao makuu na mikoa michache ili kujaza nafasi zilizokuwa wazi.


Shariff amesema kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi mkuu wa RUWASA, mhandisi Clement Kivegalo nafasi ya meneja wa Manyara ina kaimiwa na mhandisi James Kionaumera aliyekuwa meneja wa RUWASA wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani.


Amesema meneja wa RUWASA mkoa wa Katavi, mhandisi Peter Ngunula ameteuliwa kuwa kaimu meneja wa uendeshaji na matengenezo kwenye idara ya huduma za ufundi.


Amesema meneja wa RUWASA wilaya ya Lindi mhandisi Idd Pazzi ameteuliwa kuwa kaimu meneja wa RUWASA Mkoa wa Katavi.


Kwa upande wake, mhandisi Kirita amewashukuru wananchi wa Manyara na viongozi kwa namna walivyompa ushirikiano mkubwa kipindi alichokuwa akihudumu nafasi hiyo.


"Nawashukuru viongozi wa mkoa, wilaya, watumishi wenzangu wa RUWASA na wananchi wote kwa namna tulivyoshirikiana kufanya kazi kipindi chote nilipokuwa Manyara," amesema mhandisi Kirita.


Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari wa mkoa wa Manyara, Zacharia Mtigandi amemuelezea mhandisi Kirita kuwa ni kiongozi mchapakazi hivyo anastahili kupanda kwenye nafasi hiyo.


Mtigandi amesema mhandisi Kirita ni kiongozi ambaye hakuwa anakaa chini kwani kila wakati alikuwa vijijini akifuatilia miradi ya maji kwa manufaa ya jamii ya mkoa wa Manyara.


"Hata kwenye mbio za mwenge miradi ya maji ya RUWASA watu walikuwa wana uhakika itapitishwa kwa namna ilivyojengwa kwa ubora na yenye thamani ya fedha zilizotengwa zinaonekana kwa ubora," amesema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...