BODI ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) imehitimisha mafunzo kwa wataalam kutoka vyuo na taasisi wanaohusika shughuli mbalimbali za mitihani kuhakikisha viwango vipya vya mabadiliko ya mtaala vinafuatwa.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo ya siku mbili Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania ( NBAA) CPA Pius A. Maneno amesema teknolojia imebadilika hivyo na wao sasa ni wakati umefika wanatakiwa kubadilika na pia wataalamu wanapaswa kuwa mabalozi wa mabadiliko akisisitiza kuwa mitihani inapaswa kupima ujuzi halisi na sio kutumia teknolojia kama akili bandia (AI) inayoweza kutoa majibu ya nadharia, ambayo hayapimi uwezo wa mwanafunzi.
Ametoa shukrani kwa wakufunzi na washiriki wa mafunzo hayo yaliyolenga kuleta mabadiliko hasa kwa kipindi hiki cha Mtaala mpya na kuongeza kuwa elimu waliyoipata itawasaidia pia kwenda kuitumia huko vyuoni.
Maneno aliwapongeza washiriki kwa kujitolea kujifunza mbinu mpya na teknolojia zinazohusiana na utungaji wa mitihani na umuhimu wa wataalamu wa uhasibu kutumia maarifa waliyoyapata kusaidia wengine na kuboresha sekta nzima ya uhasibu nchini.
Naye mmoja wa washiriki alisema mafunzo hayo yanalenga hasa ni kwanini wanafunzi wanafeli hivyo wanaelekezwa namna nzuri ya kutunga mitihani kwa kuangalia mtaala unavyoelekeza ili kuepuka kutoka nje ya mtaala na kuweza kumpima mtahiniwa wa Bodi uelewa wake katika hatua aliyopo.
Pia mafunzo hayo yamewapa uelewa zaidi kuhusu usimamizi wa mitihani na mbinu bora za kujenga wanafunzi wenye uwezo wa kuhimili changamoto za soko la ajira kwa weledi wa kutosha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania ( NBAA) CPA Pius A. Maneno akizungumza wakati wa kufunga mafunzo kwa Wakufunzi kutoka Vyuo mbalimbali wanaofanya shughuli mbalimbali za mitihani Mafunzo yaliyofanyika katika Ofisi za NBAA jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Elimu ya Taaluma na Mafunzo NBAA, Peter Lyimo (kulia) akitoa maelezo kuhusu namna semina hiyo ilivyendeshwa kwa Wakufunzi kutoka Vyuo mbalimbali wanaofanya shughuli mbalimbali za mitihani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...