Na Mwandishi Wetu ,Mara


Serikali kupitia wizara mbili zenye dhamana ya mawasiliano na uchukuzi Tanzania bara na Zanzibar zimeanzisha mchakato wa kuridhia mikataba ya kimataifa ya kuhifadhi mazingira ya usafiri wa bahari kwa kusimamia ulinzi wa sekta hiyo pamoja na kuendesha vyombo kwa usalama.

Hayo ameyasema Naibu Katibu Mkuu wa Wizara  ya Miundombinu, Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  Makame Haji kwa niaba ya Waziri wa Miundombinu, Mawasiliano  na Uchukuzi Dkt. Khalid Salum Mohamed  wakati wa akiufungua maadhimisho ya siku ya usafiri kwa njia ya maji na miaka 50 ya IMO yaliyofanyika  Septemba 23 katika Viwanja vya Mkendo ,Manispaa ya Musoma mkoani Mara

Amesema Uharibifu wa mazingira katika upande mmoja wa dunia unaweza kuleta athari kubwa sehemu mbalimbali duniani ikiwa ni pamoja na nchini kwetu, hali inayosababisha  kuanzishwa kwa Mikataba ya Kimataifa inayohusu masuala mbalimbali ya hifadhi ya mazingira, kwa lengo la kuweka juhudi za pamoja kukabiliana na changamoto hizo na kuendelea kuhifadhi mazingira kwa pamoja kama urithi wa dunia kwa vizazi vijavyo.

Makame  ametoa rai kwa Watanzania kutunza mazingira ya usafirishaji majini ikiwa ni utekelezaji wa Mkataba Maalum wa Kimataifa wa Shirika la Bahari Duniani (IMO) unaozuia uchafuzi wa mazingira majini unaotokana na shughuli zinazofanyika katika Meli (MARPOL) .

Amesema Siku ya Bahari Duniani ni kuelimisha umma kuhusu jinsi wanadamu wanavyoathiri bahari, kuendeleza harakati za kimataifa zinazotetea bahari zetu, na kuhamasisha na kuunganisha watu duniani kote kuchukua hatua ya kuwaokoa

“Serikali tayari imesharidhia mkataba huu pamoja na kanuni zake (Annex) tano kati ya sita ilizotolewa na IMO na tumeshaanza kutekeleza mikakati yake. Kwa sasa tunajenga Kituo kikuu cha Ufuatiliaji na Uokoaji (MRCC) kwa ajili ya Ziwa Victoria ambacho kitatumika kupitia ukanda Afrika Mashariki huku akiweka bayana umuhimu wa Sekta ya Uchukuzi,” ameongeza Bw. Haji.

 Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Bahari Zanzibar (ZMA)  Mtumwa Said Sandal amesema kuwa na uwepo wa elimu ya kutosha juu ya utunzaji wa mazingira itasaidia wananchi kuwa na uelewa zaidi juu ya utunzaji na udhibiti wa usalama mazingira.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu, Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Makame Haji akizungumza wakati akifungua maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Mkendo Manispaa ya Musoma mkoani Mara.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Nahodha. Mussa Mandia akitoa maelezo kuhusiana mikakati Bodi  hiyo katika Ushauri masuala mbalimbali kwenye maadhimisho ya ya Siku ya Bahari Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Mkendo Manispaa ya Musoma mkoani Mara.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Bahari Zanzibar (ZMA) Mtumwa Said Sandal akizungumza kuhusiana na utendaji wa Mamlaka hiyo na ushirikiano wa TASAC kwenye maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Mkendo Manispaa ya Musoma mkoani Mara.
Baadhi ya viongozi mbalimbali katika maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Mkendo Manispaa ya Musoma mkoani Mara.
Picha ya pamoja ya makundi mbalimbali na mgeni Rasmi kwenye maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Mkendo Manispaa ya Musoma mkoani Mara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...