BALOZI wa Tanzania Japan Baraka Luvanda kwa mara ya kwanza amepokea shehena ya Mananasi yaliyokaushwa kutoka kimele na Mapinga katika wilaya ua Bagamoyo Tanzania ikiwa ni sehemu ya utamburisho wa zao hilo katika soko la Japan.

Balozi Luvanda amepokea bidhaa hiyo Septemba 24 , 2024 kupitia Kampuni ya Taishin Co. Ltd., ya Japan katika Bandari ya Tokyo .shehena ambayo imehifadhiwa katika Hifadhi ya bandari Kawanishi (Kawanishi Warehouse) iliyopo jijini Tokyo.

Nchi ya Japan inatarajiwa kuanza kuuza kwenye Masoko makubwa ya bidhaa (Supermarkets) ya TOMIZAWA na LIFE CORPORATION zilizoenea katika miji yote ya Japan .

Kampuni ya Taishin ya Japan ina ubia na Kampuni ya Elven Agri ya Tanzania katika kupeleka zao hilo nchini Japan ikiwa ni fursa kubwa kwa Tanzania na wakulima wa zao hilo katika kulifikia soko la Japan.

Ubalozi wa Tanzania Nchini Japani umepongeza jitihada hizo zinazofanywa na Watanzania na Japan kupitia kampuni hizo katika kufanikisha hatua hii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...