RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Viongozi walioteuliwa ni kama ifuatavyo:-
Bi. Nenelwa Mwihambi ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Kabla ya uteuzi huu, Bi. Mwihambi alikuwa Katibu wa Bunge; na
Bw. Baraka Ildephonce Leonard ameteuliwa kuwa Katibu wa Bunge. Bw. Leonard anachukua nafasi ya Bi. Mwihambi ambaye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
Viongozi walioteuliwa wataapishwa tarehe 19 Septemba, 2024 saa 09.00 alasiri, Ikulu – Dar es Salaam.
Sharifa B. Nyanga
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...