Makocha wa mchezo wa Judo wakiwa katika picha ya pamoja na Mkufuzi kutoka UWW Erdal Dogan ambaye ni raia wa Uturuki, wakiwa kwenye mafunzo yaliyoanza leo 22Septemba 2024 kwenye Kituo Cha Olympafrica Wilayani Kibaha Mkoani Pwani
Na Khadija Kalili Michuzi Tv
WALIMU 30 wa Mchezo wa Judo kutoka Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar wameanza mafunzo ya siku kumi ambayo yanaendelea katika Kituo Cha Olympafrica Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.
Katibu Mkuu Chama Cha Mchezo wa Judo Tanzania Innocent John Mallya amesema kuwa mafunzo yameanza leo 22Septemba hadi Oktoba mosi 2024 ambapo waalimu wa Judo nchini watapatiwa mafunzo na Mkufunzi UWW Erdal Dogan ambaye ni raia wa Uturuki.
Katibu Mkuu wa Judo nchini Mallya amesema kuwa hali ya mchezo wa Judo inaridhisha kwa sababu wametoka kushiriki katika michuano ya Olympic iliyofanyika Jijini Paris na kushika nafasi ya 16 bora.
Kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo katika mchezo huo amesema kuwa ni ukosefu wa vifaa vya kuwafundisha watoto kuanzia umri wa miaka saba na kuendelea.
"Mchezo huu wa Judo una ukosefu vifaa kwani hata hawa waalimu wanaofundishwa watakapo maliza mafunzo yao kitakacho wakwamisha ni uhaba wa vifaa vya kufunzishia tunaiomba serikali ikumbuke kutenga maeneo ya viwanja vya ndani vya Judo (Indoor) kwa sababu huu mchezo unachezewa ndani kama jinsi mnavyoona na pia yanahitajika magodoro maalumu ya kuchezea ambayo yanahamishika.
"Tuna vifaa vya Judo vimekwama bandarini tangu Aprili 2023 ambavyo tumepewa msaada na Chama Cha Judo Dunia ambapo tunadaiwa zaidi ya Mil.Miamoja na nane ila kutokana na jinsi ushuru kuwa unapanda kila siku itakua imezidi, awali serikali ilituahidi kutusaidia kutulipia ushuru huo lakoni sasa muda unazidi kwenda hatujaambiwa lolote awali wametupa nguo za mchezo huo zilizokuwa jozi 350 zilizokuja pamoja na magodoro ambayo bado yamekwama bandarini tunaiomba serika ikumbuke ahadi yake ya kutusaidia kupata hivyo vifaa kwani vitasaidia kuukuza mchezo wa Judo vifaa hivyo vitagawanywa katika Mikoa mbalimbali nchini" amesema Katibu Mkuu wa Judo Mallya.
Amesema kuwa mchezo wa Judo ni ajira kama zilivyo ajira nyingine pia Judo imeweza kutoa ajira kwa vijana wengi ambao wameajiriwa kwenye Majeshi nchini pamoja na taasisi mbalimbali, pili Judo ni ulinzi binafsi na ni mzuri kwa afya.
"Hii ni programu ya kuuendeleza mchezo wa Judo kwa watoto malengo ambayo tumeanzisha tangu 2023 na katika takwimu zetu zinaonesha tunawachezaji 508 hadi sasa.
Akitoa salamu za Olympic Tanzania kwenye ufunguzi wa mafunzo haya aliyekua mgeni rasmi Mwenyekiti wa TOC Gulam Rashid amewataka Makocha hao kuzingatia maelekezo yote kutoka kwa Mkufunzi huyo Mturuki Erdal Dogan.
Wakati huohuo Katibu Mkuu wa TOC na Meja Mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Filbert Bayi amesema mafunzo hayo yameandaliwa na Kamati ya TOC ikiwa ni katika mwendelezo wa mafunzo mbalimbali wanayoyaandaa pia amesisitiza kwa kusema kuwa kufuatia kukwama kwa vifaa vya Judo Bandarini suala hilo liko nje ya uwezo wa TOC, huku akivitaka vyama kutumia anuani za serikali ili kukwepa changamoto za kulipa ushuru "Hayo magodoro ya mchezo wa Judo hiyo ndiyo kama nyasi bandia kwa mchezo wa soka ambazo serikali imetoa msamaha wa ushuru hali ambayo imechangia ukuaji wa mchezo wa soka ," naiomba serikali ifikirie kutoa ushuru kwenye vifaa vyote vya michezo nchini ambavyo huagizwa kutoka nje ya nchi na kuweza kunusuru na kukuza vipaji vya michezo ukowemo Judo" amesema Bayi.
Kuhusu faida ya mafunzo haya kwa Makocha wa Judo amesema kuwa endapo kila Kocha atafundisha wachezaji wawili watakua wamepata wachezaji 60 katika mchezo wa Judo ambao ni muhimu katika maisha, nimesoma kitabu kimoja kinaeleza kuwa Rais wa Urusi ni bingwa wa Judo hii ni ninaimani kwa sababu ya ulinzi wake binafsi" amesema Bayi.
Katibu Mkuu wa TOC Meja Mstaafu wa JWTZ Filbert Bayi akizungumza na waandishi hawapo pichani katika Kituo Cha Olympafrica kilichopo Wilayani Kibaha Mkoani Pwani leo 22Septemba, 2024
Mkufunzi kutoka UWW Erdal Dogan raia wa Uturuki akitoa maelekezo kwa Kocha katika mafunzo yaliyoanza leo Kituo Cha Olympafrica Wilayani Kibaha Mkoani Pwani
Kutoka Kushoto ni Rais wa Judo Tanzania Zaidi Hamisi Omari , Mkufunzi kutoka UWW Erdal Dogan na Katibu Mkuu wa Chama Cha Judo Tanzania Innocent John Mallya
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...